Huwa
ni nadra sana kuliona tabasamu la Kanye West, lakini imedhihirika kuwa
mapenzi yake kwa mpenzi wake Kim Kardashian na mwanao North West ndio
ufunguo pekee wa tabasamu hilo.
Pia inawezekana hujawahi kumuona Kanye akiwa ‘emotional’ kama
alivyokuwa wakati wa Interview aliyofanyiwa na mkwe wake Kris Jenner
iliyoruka jana. Kanye alikubali kuwa yeye ni mtu mwenye aibu na mwoga
hasa anapokuwa mbele za watu tofauti na anapokuwa jukwaani.
Hisia za Kanye ambaye alikuwa na aibu flani zilikua zinajionesha hata
katika mahojiano hayo hasa wakati alipokuwa akiulizwa kuhusu Kim
Kardashian na North. Kanye alikuwa anachezesha mguu, anachezea vidole
(zile ishara za aibu) lakini pia alikuwa na nidhamu ya kufa mtu mbele ya
mkwe.
North West
Kati ya vitu alivyovizungumzia kuhusu Kim ni jinsi walivyokutana na
kusema alianza kumpenda Kim kabla hawajakutana so it was love at first
sight. Katika Interview hiyo ndiyo Kanye alionesha picha ya mwanae North
kwa mara ya kwanza.
Kris alimuuliza pia kama anapenda North naye aje kuwa rapper kama
yeye, Kanye alisema atampatia fursa ya kujenga uwezo katika vitu tofauti
na kisha kumuacha North mwenyewe aje kuamua kile atakachokuwa anaweza
zaidi kukifanya na kuwa wao watamsupport katika chochote atakachoamua
kufanya.
“Im gonna give her the opportunity to develop her different skills
set, and then decide you know what she likes to do the best….we will
just give the support and let her follow what she loves the most”.
Tazama mahojiano yote hapa
Post a Comment