MSANII wa filamu
nchini Rose Ndauka kwa mara ya kwanza amefanya shoo ya aina yake ya
nyimbo ya bongo fleva aliyoshirikiswa na kundi la TNG, katika tamasha la
sikukuu ya Iddi lililofanyika Dar Live jijini Dar es Salaam.
Msanii
huyo sasa ameamua kufanya muziki ambapo ameweza kushirikishwa single
inayoenda kwa jina la 'Crazy Love ' na kundi hilo ambapo siku hiyo
ilikuwa maalumu kwake kwa ajili ya kutambulisha nyimbo hiyo.
Akizungumza
na mwaandishi wa habari hii baada ya kumaliza kufanya shoo hiyo, Rose
aliweka wazi kuwa kuimba 'live' jukwaani kunatofauti na kazi ya filamu
ambayo ameizoea.
Alisema
upande wa filamu ni rahisi kurekebisha makosa endapo ukihisi kukosea
tofauti na kuimba live jukwaani kwani ukikosea hauwezi kupata nafasi ya
kurekebisha hivyo umakini unahitajika katika kazi hiyo.
"Mimi ni msanii na kuimba ni kipaji changu kingine, lakini kwenye uimbaji inahitajika umakini zaidi tofauti na nilikokuzoea" alisema Ndauka.
Aliongezea
kuwa anamshukuru mtayarishaji wa muziki P Funk kwa kuweza kutambua
kipaji chake hicho cha uimbaji na kuweza kumpa nafasi ya kushiriki
katika nyimbo hiyo.
Kundi
la hilo linaundwa na wasanii wawili akiwemo Chiwaman pamoja na 'Latino
Man', ambapo wameachia single yao ikiambata na uzinduzi .
Post a Comment