Mamlaka
ya mawasiliano nchini, TCRA inaandaa utaratibu wa kufunga simu zote
ambazo hazina viwango vya ubora stahiki kwa lengo la kuzuia uingizwaji
wa bidhaa hizo nchini ambazo zimekuwa zikiuzwa kiholela.
Meneja mawasiliano wa TCRA ‘Innocent Mungy’ amesema mamlaka hiyo kwa
sasa inazunguka nchini kutoa elimu kwa wananchi ili wazitambue simu
mbovu na madhara yake katika mawasiliano kabla ya kufikia zoezi hilo.
Zoezi litaanza kutoa tahadhari kwa wananchi kabla ya zoezi hilo ni
kutokana na matokeo ya nchi ya Kenya ambayo ilitekeleza zoezi kama hilo
Septemba mwaka jana, ambapo pamoja na malengo yao kutimia, wananchi
wengi waliathirika pamoja na baadhi ya taasisi za serikali hasa sekta ya
afya na biashara.
Ameongeza kuwa mwongozo wa kuzima simu wenye lengo la kukabiliana na
uingizwaji wa simu bandia nchini, unatekelezwa kwa mujibu wa sheria ya
mwaka 2010 ya mawasiliano ya elektroniki na posta (EPOCA) pamoja na
kanuni zake za mwaka 2011.
Source: Times Fm
Source: Times Fm
Post a Comment