AFYA:- UMUHIMU WA VYAKULA VYA JAMII YA MBOGA MBOGA MWILINI~

~~UMUHIMU WA VYAKULA VYA JAMII YA MBOGA MBOGA MWILINI~~
 A/Alleykum;
 Watu hushauriwa kula vyakula vya jamii ya mboga mboga kwa wingi. Sababu kubwa ni kutokana na faida za kiafya ambazo huletwa kutoka kwenye mboga mboga ambazo haziwezi kupatikana kutoka kwenye vyanzo vingine. Mboga zina vitamins na madini (minerals) kama vile potassium, vitamin A & C hupatikana kwa wingi kwenye mboga mboga na huhitajika mwilini kila siku ili kuusaidia kuwa na afya na kuweza kukinga au kuzuia maradhi. Virutubisho vingine husaidia kukinga moyo na figo dhidi ya maradhi na huzuia kansa.
 
Vitamini C inapatikana zaidi kwenye mboga mboga za majani ambazo zina rangi ya kijani, kama vile mchicha, kisamvu, matembele, majani ya kunde na yale ya maboga na kadhalika. Kwa upande wa vitamini A inapatikana kwa wingi kwenye karoti. 

Zaidi ya hayo, baadhi ya mboga mboga zina protini na kabohaidreti (wanga) kwa mfano mapeyasi, maharage na viazi. Nyuzi nyuzi za kilishe (dietary fibres) pia zinapatikana kwa wingi katika mboga mboga hasa mboga za majani. 

Vitamini C ni kirutubiso kinachopotea kwa haraka wakati wa upikaji wa mboga mboga. Ili kupunguza tatizo hilo, mboga mboga zipikwe kwa dakika chache, kama vile dakika tano mpaka kumi. Kwa utaratibu huu, maji yachemshwe kwanza. Yaani osha mboga zako vizuri kwa maji safi halafu zitie katika maji yanayochemka. Baada ya dakika hizo tano mpaka kumi zitakuwa zimewiva kwa kiasi ambacho hakitapoteza vitamini C kwa wingi. 

Sambamba na hatua hiyo, mboga mboga (vegetables) lazima zipikwe kwenye chombo kilichofunikwa ili vitamini zisiondoke na mvuke. Pia watu wajilazimishe kunywa ule mchuzi (supu) unaopatikana baada ya kupika hizo mboga mboga. Hii ni kwa sababu, mchuzi huo unavitamini nyingi inayotoka kwenye mboga mboga. 

Watu wanatakiwa waongozwe na elimu na wala siyo walivyozoea. Kwa maneno mengine wasione kinyaa kunywa hiyo supu ya mchuzi.~UMUHIMU WA VYAKULA VYA JAMII YA MBOGA MBOGA MWILINI~~
A/Alleykum;
Watu hushauriwa kula vyakula vya jamii ya mboga mboga kwa wingi. Sababu kubwa ni kutokana na faida za kiafya ambazo huletwa kutoka kwenye mboga mboga ambazo haziwezi kupatikana kutoka kwenye vyanzo vingine. Mboga zina vitamins na madini (minerals) kama vile potassium, vitamin A & C hupatikana kwa wingi kwenye mboga mboga na huhitajika mwilini kila siku ili kuusaidia kuwa na afya na kuweza kukinga au kuzuia maradhi. Virutubisho vingine husaidia kukinga moyo na figo dhidi ya maradhi na huzuia kansa.

Vitamini C inapatikana zaidi kwenye mboga mboga za majani ambazo zina rangi ya kijani, kama vile mchicha, kisamvu, matembele, majani ya kunde na yale ya maboga na kadhalika. Kwa upande wa vitamini A inapatikana kwa wingi kwenye karoti.

Zaidi ya hayo, baadhi ya mboga mboga zina protini na kabohaidreti (wanga) kwa mfano mapeyasi, maharage na viazi. Nyuzi nyuzi za kilishe (dietary fibres) pia zinapatikana kwa wingi katika mboga mboga hasa mboga za majani.

Vitamini C ni kirutubiso kinachopotea kwa haraka wakati wa upikaji wa mboga mboga. Ili kupunguza tatizo hilo, mboga mboga zipikwe kwa dakika chache, kama vile dakika tano mpaka kumi. Kwa utaratibu huu, maji yachemshwe kwanza. Yaani osha mboga zako vizuri kwa maji safi halafu zitie katika maji yanayochemka. Baada ya dakika hizo tano mpaka kumi zitakuwa zimewiva kwa kiasi ambacho hakitapoteza vitamini C kwa wingi.

Sambamba na hatua hiyo, mboga mboga (vegetables) lazima zipikwe kwenye chombo kilichofunikwa ili vitamini zisiondoke na mvuke. Pia watu wajilazimishe kunywa ule mchuzi (supu) unaopatikana baada ya kupika hizo mboga mboga. Hii ni kwa sababu, mchuzi huo unavitamini nyingi inayotoka kwenye mboga mboga.

Watu wanatakiwa waongozwe na elimu na wala siyo walivyozoea. Kwa maneno mengine wasione kinyaa kunywa hiyo supu ya mchuzi.

Post a Comment

Previous Post Next Post