
Ofisa
Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Kampuni ya Vodacom Hassan Saleh
akimkabidhi Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Pandu Ameir Kificho
kombe lililotolewa na Vodacom kwa ajili ya mshindi wa mechi maalum kati
ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Wabunge wa Bunge la Tanzania
kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Mchezo huo ulichezwa
kwenye Uwanja wa Amaan Mjini Zanzibar na kufadhiliwa na Vodacom
Tanzania.

.Spika
wa Baraza La Wawakilishi Pandu Ameir Kificho akilikagua kombe
lililotolewa na Kampuni ya Vodacom kwa ajili ya mshindi wa mechi maalum
kati ya Timu ya Soka ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Wabunge wa
Bunge la Tanzania kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Mchezo
huo ulichezwa kwenye Uwanja wa Amaan Mjini Zanzibar na kudhaminiwa na
Vodacom. Timu ya Bunge ilishinda bao moja kwa bila.

Spika
wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar Pandu Ameir Kificho akimkabidhi
Nahodha wa Timu ya Soka ya Wabunge wa Bunge la Tanzania Amos Makala
amabe pia ni Naibu Waziri wa Habari,Vijana Utamduni na Michezo kombe
kufuatia kuichapa timu ya Baraza la Wawakilishi kwenye mechi maalum ya
kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Katikati ni Ofisa Mkuu wa
Mauzo na Usamabazaji wa Vodacom Hassan Saleh waliodhamini mechi hiyo
iliyopigwa kwenye Uwanja wa Amaan Mjini Zanzibar.

Kikosi
cha Timu ya soka ya Wabunge wa Bunge la Tanzania kikiwa na kombe muda
mfupi mara baada ya kukabidhiwa baada ya kuifunga timu ya Baraza la
Wawakilishi bao moja kwa bila kwenye mechi maalum ya kusherehekea mika
50 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Mchezo huo ulidhaminiwa na kampuni ya
Vodacom.
Kikosi
cha Timu ya Netiboli kinachoundwa na Wabunge wa Bunge la Uganda kikiwa
katika picha ya pamoja muda mfupi kabla ya kushuka uwanjani kuvaana na
kombaini ya Zanzibar ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya
Mapinduzi ya Zanzibar. Katikati ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom
Salum Mwalim.
Post a Comment