Kampuni Ya Google Iko Mbioni Kutoa Smart Contact Lenses

gl
Kampuni kubwa inayo ongoza katika maswala ya Technology ulimwenguni Google, wapo katika maandaliza ya kuzindua bidhaa yao mpya aina ya lens za macho ijulikanayo kama Smart Contact Lenses. Lens hizo za macho hazijatengenezwa kwa ajili ya watu wenye matatizo ya macho na wala si kwa ajili ya internet au mawasiliano ya aina yeyote kama watu wanavyodhania bali ni lens ambazo zitakuwa zikitumika kuangalia kiasi cha sukari mwilini.
gl2
Lens hizo zimetengenezwa haswa kwa ajili ya watu wanaosumbuliwa na ugonjwa wa kisukari. Kupitia lens hizo wagonjwa wataweza kupima kiurahisi kiasi cha sukuari mwilini mwao kupitia ute/machozi katika macho, na kwa sasa kampuni ya hiyoo ya Google iko katika majaribio ya matumizi ya lens hizo baada ya kufanya research za kisayansi za kutosha na pia wanatafuta kampunia ambayo itaweza kuungana nayo kwa ajili ya kuziachia bidhaa hizo katika soko.

Post a Comment

أحدث أقدم