Hit maker wa ‘Nakula Ujana’ Nay wa Mitego amesema mwaka huu ana
collabo 3 ambapo moja ameanza na kufanya na mwanadada NeyLee katika
wimbo‘Usinikatae’ utakaotoka hivi karibuni.
“Nimeanza kurekodi ngoma mpya na Ney Lee nikagundua kumbe ni demu
fulani ambae anaweza sana halafu kama hana msaada hivi,” Nay ameiambia
Bongo5. “Kwahiyo baada ya kuona uwezo wake katika wimbo ambao nimefanya
naye (Usinikatae) nimeamua kumpa tafu na nitajitahidi kumpushi kidogo
kwa namna yoyote kwasababu mimi kidogo nipo mbele yake. KwaHiyo nadhani
hivi karibuni ngoma itakuwa inatoka. Hii ngoma ni kali sana,” ameongeza
rapper huyo.
“Ney Lee ni msanii ambaye anasimamiwa na watu na mimi namsimamia
katika huu wimbo pekee, kwasasabu namchukulia kama dada yangu,
alikotokea na alikotokea mama yangu ni kumoja,pia anaweza sana,kwa watu
ambao wanamsaidia wataendelea kumsaidia, kila mtu atasaidia kwa nafasi
yake. Nimeshaanza kuongea na directors wa video kwasababu hii ngoma siyo
ya kuiacha pekee bila video hata baada ya kumaliza kurekodia watu wa
studio wakaanza kusema ‘acheni iende kwanza’ ila sisi tukaona bora
tusubirie tujue director wa video atasemaje then tutajua tuiachie ama
vipi.”
Kuhusu collabo na Diamond, Nay amesema bado hajajua ni ngoma ipi atakayoitoa. “Kuna nyimbo 3 ambazo nimefanya na
Diamond, kwahiyo tunaweza tukaiachia au lah, kwasababu tunataka ikija iwe na video full, vyote vinawezekana.”
Diamond, kwahiyo tunaweza tukaiachia au lah, kwasababu tunataka ikija iwe na video full, vyote vinawezekana.”

Post a Comment