Muigizaji aliyehamia kwenye muziki, Snura anatarajia kuachia
wimbo mpya ‘Ushaharibu’ kabla ya kutoa album ya Majanga pamoja na filamu
yake.
Snura akiongea na Clouds FM weekend hii, Snura alisema kwenye video
ya ‘Nimevurugwa’ kuna chorus ya ‘Ushaharibu’ ambayo imefanya shabiki
wake wamuulizie kama anataka kuachia wimbo kama huo.
“Muziki kinachofuata ni ‘Ushaharibu’ kama watu ambavyo wameona video
yangu nimevurugwa ina chorus ya ‘Ushaharibu’ watu wamekuwa wakiniulizia
sana kuhusiana na hiyo ngoma. Ni ngoma ambayo imependwa kabla hata
ijatoka. Kwahiyo sasa hivi najiandaa kuiachia hiyo ngoma lakini mtaani
kuna ngoma niliachia kama zawadi kwa wapenzi wa taarab inaitwa ‘Huko
Nyuma’ kwahiyo ningependa kuitoa sasa hivi ‘Ushaharibu’ nitakuwa kama
napandisha vitu juu yake. Najaribu kuvuta muda kidogo halafunitaiachia,”
alisema.
“Natarajia kuachia album ambayo itakuwa na mseto wa kutosha ikiwemo
hiyo nyimbo ya taarab ,tutakuwa na mduara,kutakuwa na afro pop na nyimbo
ambazo zitakuwa tofauti tofauti yaani ya album ya Majanga itakuwa na
nyimbo tofauti tofauti na ndani ya mwaka huu nitaachia album na filamu
ya Majanga.”

Post a Comment