MISS TANGA 2014, YAZINDULIWA LEO!

10389276_917797848234634_8865585498372923951_n
Shindano la kumsaka mlimbwende wa Jiji la Tanga, Nice and Lovely Miss Tanga 2014 leo hii limezinduliwa rasmi Jijini Dar es Salaam, sambamba na kutambulishwa kwa zawadi kubwa kwa mshindi, Gari aina ya Totota Vits yenye thamani ya shilimgi milioni 10.
Msemaji wa Kamati ya maandalizi Nice & Lovely Miss Tanga 2014, Bi Regina Gwae ametoa wito kwa warembo wa Mkoa wa Tanga kujitokeza kwa wingi kushiriki katika kinyangayiro hiki kitakachofanyika tarehe 21 mwezi Juni.
Washiriki wa Shindano hili wanatarajia kuingia kambini tarehe 9 mpaka tarehe 20 mwezi wa 6 ambayo itakuwa ni siku moja kabla ya shindano.
Wadhamini wa mashindano haya makubwa kituo cha EATV Ting’a Kali Namba moja kwa Vijana pamoja na East Africa Radio kupitia afisa masoko wake Bi. Happy Shame, wakiwa na lengo la kunyanyua vipaji vya vijana, amewataka wapenzi wa masuala ya ulimbwende Tanga kufurahia mashindano haya kupitia udhamini huo mnono.
Fomu kwa warembo wanaotaka kushiriki mashindano haya zinapatikana Mkonge Hotel, D-Boutique Tanga Mjini, Tanga Beach Resort, Five Brothers, Sophia Records, Danny Fashion barabara ya 13, Ofisi za The Guardian Tanga Barabara ya 15, Yolanda Salon Mtaa wa Eckenford na Nyumbani Hotel.

Post a Comment

أحدث أقدم