NGULI wa
filamu za Kibongo, Jacob Steven ‘JB’, amesema kuwa pamoja na kuendelea
kulia juu ya kuibiwa kazi zao, anamkumbusha Rais Jakaya Kikwete kutimiza
ahadi yake aliyowahi kusema kwenye msiba wa nguli wa filamu, Steven
Kanumba kuwa atawashungulikia wale wote wanaoiba kazi za wasanii na
kutoa kopi.
Nguli wa filamu za Kibongo, Jacob Steven ‘JB’.
JB alitoa ombi kwa uchungu ambapo alifunguka kuwa pamoja na kuwepo kwa
wasambazaji lakini bado wasanii wamekuwa wakilia kila siku hasa pale
wanapopeleka filamu zao sokoni.
“Rais wetu alitoa kauli kuwa anawashungulikia wale wote wanaohusika na
wizi wa kazi zetu, lakini hadi leo bado hajatekeleza hilo, lakini
hatuwezi kushindwa kusema kuwa tunaumia sana, tunaomba atusaidie,”
alisema JB.

Post a Comment