Wabunge wawili wa chama cha NCCR-Mageuzi, wamekanusha kuwa na mkakati
wa kukihama chama hicho na kwenda kujiunga na chama cha ACT-Tanzania.
Wakizungumza jijini Dar es Salaam jana, wabunge hao David Kafulila
(Kigoma kusini) na Felix Mkosamali (Muhambwe), walisema taarifa
iliyotolewa na kiongozi mmoja wa ACT kwamba wanataka kuchukua hatua hiyo
ni njia ya kujitangaza kupitia wao.
Mkosamali alisema binafsi amezisikia taarifa za yeye kuhusishwa
kuhama chama hicho, lakini amelipuuza kutokana na kwenda kinyume na
dhamira yake ndani ya chama.
Alisema hashangai viongozi wa ACT kutamka maneno ya aina hiyo,
kwani chama chao bado kichanga na wanatumia majina ya viongozi
mbalimbali kujitangaza kwa wananchi ili wafahamike.
“Nataka kuwashauri ACT kama wanataka kujitangaza watumie njia
nyingine, lakini kueneza maneno ya uongo eti nina mpango wa kuondoka
NCCR-Mageuzi watakuwa wanajisumbua,” alisema Mkosamali.
Mbunge huyo aliongeza kwamba wananchi wa jimbo lake wamemchagua
kuwa Mbunge baada ya kuridhika na uimara wa chama hicho, hivyo hawezi
kuwasaliti kwa kuondoka na kwenda katika chama ambacho hakifahamiki.
Kwa upende wa Kafulila, alisema kama jambo hilo lingekuwa na
ukweli, asingefanya kazi ya kukiimarisha kwa kufungua matawi katika
jimbo lake.
“Sauti yangu haipo sawa kutokana na kufanya kazi kubwa ya kuongea
na Wananchi pamoja na kufungua matawi katika jimbo langu, niliposikia
jambo hili nilisikitika sana,” alisema kafulila.
Hata hivyo, aliwataka wananchama wa chama hicho kutosikiliza maneno
ya mitaani, badala yake wajikite katika kujenga umoja hasa katika
kipindi hiki ambacho chafuzi mbalimbali zinatarajia kufanyika

إرسال تعليق