Arsenal
wamepoteza kwa ncha nafasi ya kufanya maajabu kwenye Champions League
baada ya kushuhudia bao zao 2-0 dhidi ya Monaco kwenye uwanja wa Stade
Louis II zikishindwa kuwavusha kwenda hatua ya robo fainali.
Wikiwa
wamefungwa 3-1 Emirates Stadium katika mchezo wa kwanza, Arsenal
walihitaji ushindi wa bao 3-0 ili kusonga mbele na matumaini ya wageni
yaliongezeka baada ya Ramsey kufunga bao la pili dakika ya 79.
Bao
la kwanza la Arsenal liliwekwa kimiani na Giruod katika dakika ya 36 na
kama vijana wa Arsene Wenger wangefanikiwa kupenya, basi ingekuwa timu
ya kwanza kufanya hivyo tangu mwaka 1969 wakati Ajax ilipotoka nyuma kwa
tofauti ya bao mbili kwenye uwanja wao wa nyumbani na kusonga mbele
baada ya mchezo wa marudiano ugenini kwenye European Cup.
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
Post a Comment