Mitandao ya kijamii imeanza kuchukua nafasi na hata kuwa sehemu
ya maisha ya kawaida, watumiaji wake hupata taarifa mbalimbali na pia
nafasi ya kuanzisha mijadala motomoto.
Hata hivyo, changamoto kubwa iliyopo katika
mitandao hiyo ni ugumu wa kudhibiti mijadala, hivyo wakati mwingine
taarifa nyingine zinakosa ukweli na kuhitaji vyanzo zaidi ili
kuzithibitisha.
Suala la Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe
kushindwa kesi na hatimaye kuvuliwa uanachama na chama chake cha
Chadema, limekuwa sehemu ya mjadala na malumbano makali katika mitandao
ya kijamii.
Ili taarifa iaminiwe na wasomaji, mitandao mingi
ilinukuu akaunti ya ‘twitter’ ya Kituo cha redio cha East Africa
kilichoitoa taarifa ya Zitto kama habari mpasuko.
Katika taarifa hiyo, alinukuliwa Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu akitangaza rasmi Zitto kuvuliwa uanachama.
Katika baadhi ya mitandao majibizano kati ya
watetezi wa Zitto na upande wa pili, yalionyesha kama makundi hayo
yangekuwa ukumbini kuna tukio baya lingeweza kutokea kwa upande mmoja
kushindwa kujizuia na kuanzisha mapigano.
Hii inatokana na ukweli kwamba mbunge huyo ana
mashabiki wengi kwenye mitandao ya kijamii na pengine ni miongoni mwa
wanasiasa wachache wanaojitokeza hadharani kwenye mitandao na kushiriki
mijadala bila woga.
Kama kuna suala linalohitaji ufafanuzi kutoka kwa
Zitto, mashabiki wake hawalazimiki kusubiri kauli yake kwenye magazeti
kesho yake kwa kuwa hachelewi kutoa maelezo kupitia kwenye akaunti zake
kwenye mitandao.
Hata baada ya uamuzi wa Mahakama Kuu iliyotupilia
mbali pingamizi lake la kutaka asijadiliwe na chama chake, baada ya muda
mfupi Zitto aliibuka katika mitandao ya kijamii akitoa ufafanuzi wa
kilichotokea.
“Hatukuwa na wito wa Mahakama leo. Jaji
kahamishiwa Tabora. Hatuna taarifa ya Jaji mpya. Mwanasheria wetu
anafuatilia na atatoa maelezo,’’ alisema kupitia mtandao wa Twitter.
Uandishi wake kwa kiwango kikubwa ulikidhi
mahitaji ya watumiaji wa mitandao ya kijamii ambao wengi hupenda kusoma
sentensi fupi fupi na zinazoeleweka kuliko maelezo marefu yenye ajenda
tofauti.
Mwigulu Nchemba aibuka

إرسال تعليق