NYOTA
wa filamu za Kibongo Lungi Maulanga hivi karibuni anadaiwa kutupiwa
jini na wabaya wake wakiwemo wanafamilia yake kitendo kilichosababisha
apooze upande mmoja wa mwili wake.
Nyota wa filamu za Kibongo Lungi Maulanga.
Chanzo makini kinasema hofu yao kubwa ni kuwa kitendo hicho
kilifanywa na baadhi ya ndugu zake kufuatia tofauti zao za kifamilia
zilizosababisha kufikishana mahakamani.
“Katika shauri hilo mahakamani, yeye alishinda, sasa baada ya siku
mbili akaanguka na kupoteza fahamu, alipozinduka akajikuta amepooza
upande wa kulia, watu wanaunganisha tukio hilo na kesi ya mahakamani,”
kilisema chanzo.
Gazeti hili lilimkuta Lungi akiwa amelala nyumbani kwake na alikiri
kuanguka na kupooza na kwamba hawezi kutembea vizuri lakini anamtumaini
Mungu kuwa hali yake itakaa vizuri kwani hana imani na mambo ya
kishirikina

Post a Comment