Ukizungumzia
mashujaa wa nchini Afrika Kusini hutaacha kumtaja Tata Nelson Mandela,
ni kweli ila yupo huyu alikuwa anaitwa Sarah Bhartman, kama ulikuwa
humjui leo blog hii inakufichulia.

Sarah alizaliwa mwaka 1789, huko Afrika kusini na kufariki mwaka 1815 huko jijini paris Ufaransa akiwa na umri wa miaka 26.
Sara alikuwa anatoka kabila la khoisan na alikuwa amejaliwa kuwa na umbo la kibantu hasa makalio makubwa.
Alikuwa ni mtumwa huko Afrika
kusini lakini baadaye akaja kuuzwa kwa Dr. Duniop baada dr huyu kuona
fursa ya biashara katika mwili wa sarah.


Sarah alitumika kama sehemu ya
maonesho ambapo wazungu walilipa viingilio kuja kuangalia lile umbo la
kibantu hasa ngozi nyeusi na makalio makubwa na kwa sababu haikuwa
kawaida kwa mabinti wa kizungu kuwa na maumbile kama yale.
Pia mmiliki wa Sarah alikuwa
akimuuza (sex slave) kwa wanaume ambao walitamani kufanya nar ngono,
hivyo mmiliki alijitengenezea pesa nyingi.

Sarah alifariki kwa ugonjwa wa
zinaa akiwa na miaka 26 na hata baada ya kufariki viungo vyake vya
mwili vilikatwa na kuwekwa kwenye makumbusho huko Paris ili wazungu
waendelee kujionea umbo lile la kibantu.
Baadaye viungo vyake vya mwili vilirudishwa Afrika kusini na kuzikwa
إرسال تعليق