Na Andrew Chale wa modewji blog
Huenda umesikia mengi juu ya watu wenye uwezo mkubwa wa kiakili na ufahamu hasa wa mambo ama IQ kubwa.
Kwa
Tanzania mtoto mwenye IQ kubwa kwa ni Mtoto Nice Valentino mwenye umri
wa miaka 3, (Pichani) ameweza kuonesha uwezo mkubwa wa kukariri mambo.
kwa
mujibu wa kituo cha Cloud FM cha Tanzania, kimenukuu maelezo kadhaa
ikiwemo ya Baba wa mtoto huyo, alieleza kuwa, mtoto huyo alianza
kuonesha uwezo tokea akiwa na miezi sita (mtoto mchanga) kwa kufanya
vitu vilivyoonesha ishara ya uwezo wa jambo.

Miongoni
mwa mambo ambayo yanafanya mtoto Nice kuwa na IQ kubwa ni uwezo wake
wa kuongea kiingereza kwa kuhesabu, kusoma na kufanya mambo kadhaa.
“Mtoto
wangu ana uwezo wa kuhesabu kuanzia moja hadi 20, wakati hajasoma hata
darasa moja. pia anaweza kuhesabu vitu vingi” alieleza baba huyo.
Mtoto
huyo Nice Valentino mwenye miaka 3 ametokea wilaya ya Kiteto mkoa wa
Manyara. Hajasoma wala kufundishwa na yoyote ila anafahamu hesabu na
anaongea Kiingereza tu.
Taarifa hii kwa msaada wa Cloud FM, kupitia kipindi cha Power Breakfast.



Post a Comment