Chini chini, idadi ya wanaotaka kugombea nafasi hii inaongezeka. Wengine wanataka wenyewe, wengine wanasakiziwa.
Ukweli ni kwamba, ingawa nafasi ya urais ni moja tu, wanaoitamani ni wengi kupindukia.
Vyama vingine vimebaki kimya, si kwamba vinazuia
mtu kujitangaza labda ni mbinu za kutaka kusubiri kwanza kuona chaguo la
CCM ili wajipange. Ila bado hatujasikia tamko la kuwazuia wanachama wa
upinzani kujitokeza kugombea kama tunavyosikia kutoka CCM.
Unaweza kuiba, wakafumba macho, unaweza kukosa
uzalendo, wakafumba macho, unaweza kushindwa kuwajibika wakafumba macho,
unaweza kutoa roho ya mtu wakafumba macho, lakini ukitangaza kugombea
urais kabla ya muda, unawekwa kifungoni. CCM wanashangaza!
Ukali wanaouonyesha kwa watu wanaojitangaza mapema
unatisha. Wangekuwa wakali kwa mambo mengine ya msingi, Taifa letu
lingekuwa mbele zaidi.
Mwaka jana, CCM iliwafungia wanachama wake sita waliojitokeza kujitangaza kugombea.
Wakapata adhabu ambayo hadi leo ni kama inaendelea
maana, hakuna uwazi. Katika dunia ya leo ya sayansi ya teknolojia, bado
mambo yanaendeshwa kama uchawi vile.
Tukihesabu siku, zinakwenda. Tungependa kuwafahamu
wagombea, tungependa kuwahoji na kuyachunguza maisha yao, kuchunguza
imani zao za mambo mbalimbali.
Ni muhimu kufahamu mtu anayetaka kugombea uongozi
wa juu katika Taifa anaamini nini? Ana itikadi gani? Anafuata sera gani?
Ni mzalendo au ni kibaraka? Yote haya ni muhimu kufahamika mapema.
Ushawishi wa wananchi
Wagombea wa CCM, hawatoki mwezini. Ni watu
wanaoishi kwenye jamii yetu. Tunawafahamu. Hivyo CCM, haiwezi kukwepa
ushawishi wa wananchi.

Post a Comment