MAMBO mengine ni ya kuyasikia yakiwatokea wenzako na usiombe
yakakukuta kama ilivyomtokea msichana huyu ambaye hakufahamika jina lake
mara moja baada ya kuchukua kipigo ‘hevi’ ambacho nusura apoteze maisha
yake, maeneo ya Sinza Afrikasana, juzi Jumatatu.
Dada huyo akilia baada ya kupokea kichapo kikali.
Mashuhuda wa tukio hilo wanasema, binti huyo akiwa na mwanaume mmoja,
walionekana wakitoka katika baa iitwayo Kona, wakiongozana hadi kwenye
baa nyingine iliyo maeneo ya Afrikasana ambako waliendelea na kinywaji.
“Yule msichana ni mmoja wa wanaojiuza pale Kona, nadhani walikuwa na
makubaliano ambayo wamefikia, maana walikuwa wakinywa kwa raha zao,
ghafla tukasikia wanaanza kuzozana, jamaa alikuwa anataka waondoke,
bibie akawa analeta longolongo,” alisema dada mmoja aliyekuwa eneo la
tukio.
Wasamalia wema wakimsaidia.
Inadaiwa kuwa dada huyo alianza kupiga yowe akitaka apewe kiasi cha
shilingi 30,000, ndipo mwanaume huyo ambaye alitoweka haraka, alipoamua
kumpa kipigo kikali kiasi cha kumpasua kichwani na kumsababishia maumivu
makali.
Akiwa amelala.
Baada ya kupokea kipigo hicho, baadhi ya wahuni walifika eneo hilo na
kuendelea kumfanyia vitendo vya kidhalilishaji hadi akina mama wa eneo
hilo walipoamua kumhifadhi kwa kumfunika kanga, lakini katika hali ya
kushangaza, msichana huyo alipitiwa na usingizi mzito.Kuona hivyo,
majirani hao waliamua kumpeleka polisi ambako hata hivyo alifukuzwa kwa
kile kilichodaiwa kuwa ni mlevi.

إرسال تعليق