BERKO, AUMIA TENA
Yaw 'Poster' Berko |
KIPA namba moja
wa mabingwa wa soka wa Afrika Mashariki na Kati wa Young Africans
Sports Club (YANGA), Yaw Berko amepewa mapunziko ya siku tano kufuatia
kuchanika katika paji la uso wakati wa harakati za kuokoa mpira katika
mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika leo Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na www.youngafricans.co.tz ,Daktari
wa timu Juma Sufian amesema mchezaji huyo ameshonwa jumla ya nyuzi tano
katika paji lake la uso hivyo atakuwa chini ya uangalizi kwa kipindi
cha siku tano kuanzia kesho akiwa katika mapunziko.
Berko aliumia
wakati akiwa katika harakati za kuokoa krosi iliyochongwa na golikipa
mwenzake na kuweza kujigonga katika mlingoti wa goli na kusababisha
kuchanika na kuweza kupata matibabu ya haraka uwanjani hapo.
Mchezaji
mwingine aliyeumia katika mazoezi hayo siku ya leo ni Hamis Kiiza Diego
ambaye aliumia katika eneo la kidevu baada ya kombora lililoachiwa na
mshambuliaji mpya Said Bahanuzi kutua karibu na kidevu chake na
kusababisha mchezaji huyo kugaagaa hadi alipopatiwa matibabu na
kuendelea na mazoezi hayo.
Mchezaji majeruhi ambaye hakuweza kufanya mazoezi hayo ni Nurdine Bakari aliyeumia mwanzoni mwa wiki hii.
Post a Comment