DOM YAENDELEA KUTISHA COPA COCA COLA
DODOMA imeendeleza wimbi la ushindi kwenye michuano ya Copa
Coca-Cola 2012 baada ya leo asubuhi (Juni 27 mwaka huu) kuifunga Mbeya mabao
2-0 katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Tamco ulioko Kibaha mkoani Pwani.
Mabao ya Dodoma katika mechi hiyo ya kundi C yalifungwa na
Japhet Lunyungu dakika ya 59 wakati Frank Kaji aliwahakikishia ushindi washindi
dakika saba kabla ya filimbi ya mwisho baada ya kupachika bao la pili.
Nayo Mjini Magharibi iliifunga Iringa mabao 3-0 katika mechi
ya kundi B iliyochezwa leo asubuhi kwenye Uwanja wa Nyumbu mkoani Pwani.
Mechi za asubuhi zilizokuwa zichezwe leo kati ya Arusha na
Kusini Pemba kwenye Uwanja wa Tanganyika Packers na Pwani na Tabora kwenye
Uwanja wa Karume sasa zitachezwa kuanzia saa 8 mchana kutokana na kutokuwepo
mawasiliano ya barabara asubuhi (Morogoro Road) kutoka mkoani Pwani kuingia Dar
es Salaam.
Leo jioni kutakuwa na mechi kati ya Rukwa na Ruvuma
(Tanganyika Packers), Mwanza na Tanga (Nyumbu), Kaskazini Unguja na Mara
(Tamco) na Singida na Kagera (Karume).
Post a Comment