MABINGWA
wa Kombe la Kagame, Yanga ya jijini Dar es Salaam, watamtangaza kocha
wao mpya Ijumaa wiki hii, ambapo ataanza kazi rasmi mara baada ya
michuano ya Kombe la Kagame baadaye mwezi ujao.
Kwa maana hiyo, Kocha Msaidizi, Fred Minziro ndiye atakayeketi kwenye benchi na kuiongoza timu hiyo inayovaa jezi za rangi ya njano na kijani kutetea taji hilo.
Kwa maana hiyo, Kocha Msaidizi, Fred Minziro ndiye atakayeketi kwenye benchi na kuiongoza timu hiyo inayovaa jezi za rangi ya njano na kijani kutetea taji hilo.
Awali,
Yanga ilibainisha kuwa inasaka kocha mwenye uzoefu na soka la Afrika
pamoja na mazingira yake kama ilivyokuwa kwa kocha aliyeondoka, Kostadin
Papic raia wa Serbia.
Kiongozi wa usajili wa Yanga, Seif Ahmed alithibitisha kuwa kocha toka Ubelgiji, Tom Saintfiet ni miongoni mwa wawili wenye nafasi kubwa kutua Jangwani.
Kiongozi wa usajili wa Yanga, Seif Ahmed alithibitisha kuwa kocha toka Ubelgiji, Tom Saintfiet ni miongoni mwa wawili wenye nafasi kubwa kutua Jangwani.
Na kwa upande wa Katibu
wa Yanga, Selestine Mwesigwa ambaye ndiye Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo
kwa sasa, alisema kuwa majina ya makocha watatu yameshapitishwa.
"Kulikuwa na maombi ya makocha 25, baada ya mchujo tumechagua makocha watatu ambao tunawachuja na kumtangaza mmoja wiki hii," alisema.
"Kulikuwa na maombi ya makocha 25, baada ya mchujo tumechagua makocha watatu ambao tunawachuja na kumtangaza mmoja wiki hii," alisema.
Alisema
timu inaendelea na mazoezi kwenye Uwanja wa Kaunda tayari kwa maandalizi
ya michuano ya Kombe la Kagame itakayoanza Julai 14 kwenye Uwanja wa
Taifa jijini Dar es Salaam.
Wakati huohuo, Kelvin Yondani
aliyejiunga Yanga toka Simba, amesema katika kipindi kifupi alichofanya
mazoezi klabu yake hiyo mpya, amebaini kuwa hakufanya makosa kutua
Jangwani.
Yondani alisema kuwa, maisha ya Jangwani ni mazuri hasa
ukizingatia kuwa amepata mapokezi na ushirikiano mzuri na wachezaji na
viongozi.
Pia ametumia fursa hiyo kuitaka Simba kumsahau kwani
yeye tayari ni mali ya Yanga na hakuna jitihada zozote za kujaribu
kumrudhisha Simba zitakazofanikiwa.
Uhamisho wa Yondani ulizua utata mkubwa baada ya klabu yake ya zamani kudai ni mchezaji wao halali, huku Yanga na mchezaji wenyewe wakisema tofauti.
Uhamisho wa Yondani ulizua utata mkubwa baada ya klabu yake ya zamani kudai ni mchezaji wao halali, huku Yanga na mchezaji wenyewe wakisema tofauti.
"Sifahamu kwanini
Simba bado wanazungumza mambo haya. Mimi nimeshamaliza kila kitu na
Yanga, ni vizuri wakaniacha nifanye kazi Yanga," alisema Yondani
Post a Comment