KOCHA WA UHOLANZI VAN MARWIJK AJIUZULU

KOCHA WA UHOLANZI VAN MARWIJK AJIUZULU

Bert van Marwijk amejiuzulu kuwa kocha wa Uholanzi kufuatiwa timu ya wadachi kutofanya vizuri kwenye michuano ya Euro 2012.

Van Marwijk na vijana wake walienda Poland na Ukraine wakiwa wanapewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa kufuatia kuwa na mafanikio kwenye World Cup 2010 nchini South Africa.

Lakini walishindwa kufikia mategemeo yaliyokuwepo baada ya kufungwa kwenye mechi zote 3 za Group B dhidi ya Denmark, Ujerumani na Portugal.

Kocha huyo wa zamani wa Feyenoord na Borussia Dortmund aliichukua Uholanzi kutoka kwa Marco van Basten baada ya Euro 2008.

Alisaini mkataba wa muda mrefu na chama cha soka cha Uholanzi (KNVB) mwezi wa 12 mwaka jana ambao ungeisha mwaka 2016.

Lakini kufuatia kufanya vibaya kwenye Euro, huku ripoti zikisema kwamba hakuwa kwenye mahusiano mazuri na wachezaji wakubwa kwenye timu kumepelekea Van Marwijk awe historia.

Post a Comment

Previous Post Next Post