WAKATI joto la uchaguzi wa klabu ya Yanga likizidi kupanda, Kamati ya
Uchaguzi ya klabu hiyo, imesema itatumia teknolojia ya kompyuta wakati
wa kupiga na kuhesabu kura.
Uchaguzi mdogo wa Yanga unaosubiriwa kwa hamu unatarajia kufanyika jijini Dar es Salaam Julai 15 mwaka huu.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Kamati ya Uchaguzi ya Yanga, Francis Kaswahili alisema mpango wa matumizi ya teknolojia hiyo una lengo ya kuongeza ufanisi na kuepukana na udanganyifu.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Kamati ya Uchaguzi ya Yanga, Francis Kaswahili alisema mpango wa matumizi ya teknolojia hiyo una lengo ya kuongeza ufanisi na kuepukana na udanganyifu.
Kaswahili,
alisema iwapo zoezi hilo litafanikiwa kama wanavyotarajia, litawezeshwa
kupigwa hatua muhimu ndani ya klabu hiyo."Kimsingi tumepanga kufanya
uchaguzi kwa ufanisi kabisa na ili kuhakikisha hilo linafanikiwa
tutatumia tekonolojia ya kompyuta," alisema Kaswahili.
"Ni
utaratibu mzuri na utakaoleweka kirahisi. Wanachama watapiga kura na
kisha kura hizo kuhesabiwa kwa mfumo huohuo wa Kompyuta."
Alisema
msingi mkubwa wa kutumia utaratibu huo ni kuhakikisha suala la
udanganyifu linakosa nafasi na pia kuharakisha zoezi lenyewe la kupiga
kura.Alipoulizwa kuhusu gharama za kuandaa mfumo huo, Kaswahili
alisema:"Baada ya siku chache zijazo ukinifuata nitajua gharama halisi
zitakazotumia."
"Hakuna shaka hilo linawezekana kwa sababu, siku
hizi siyo kama zamani kwamba kila kitu lazima kitoke Ulaya,vitu vingi
sasa vinapatikana hapa kwetu," aliongeza.Kaswahili alisema kuwa, kwa
kuanzia kamati yake itaboresha daftari la wapiga kura ili kujua idadi ya
wanachama wanaostahili kupiga kura.
"Kwanza kabisa ni lazima
tuboreshe leja, lazima tujue nani yuko hai na nani amekufa ili tupate
idadi kamili wanaostahili kupiga kura," alisema Kaswahili.Uchaguzi mdogo
wa Yanga unafanyika kuziba nafasi kadhaa ikiwamo ya Mwenyekiti, Makamu
na wajumbe wa Kamati ya Utendaji.
Aliyekuwa mwenyekiti wa klabu,
Llyod Nchunga alitangaza kuachia ngazi mapema mwezi huu baada ya
shinikizo la muda mrefu toka baadhi ya wanachama waliomtaka kufanya
hivyo.
Post a Comment