Ilikuwa June 26.2007 tulipompoteza Mh. Amina Chifupa Mpakanjia. Ikiwa pia ni siku ya upigaji vita matumizi ya madawa ya kulevya.
Amina
leo ametimiza Miaka Mitano sasa tangu alipotutoka na ataendelea
kukumbukwa kwa ucheshi wake, mbwembwe zake katika utangazaji wake
kupitia kipindi cha Chuchuchu, Kwa raha zetu, Bambataa na Leo tena
katika Redio ya Clouds FM.
Mpaka anakumbwa na mauti alikuwa
Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).Watanzania
wataendelea kumuenzi na atakumbukwa kwa vita yake dhidi ya wauzaji wa
dawa ya kulevya.
Wakati leo tukimkumbuka Bi. Amina Chifupa, serikali nayo inaadhimisha Siku ya Kupambana na Dawa za kulenya Nchini.
Pumzika kwa Amani Amina Chifupa!
Chini
ni picha za baadhi ya matukio mbalimbali ambayo Amina chifupa aliweza
kushikiriki wakati wa Uhai wake. Picha Hizi zilipigwa enzi hizo na John
Badi wa Daily Mitikasi Blog |
Post a Comment