MZIMU wa Muungano umeibuka tena bungeni jana baada ya mbunge wa
Micheweni, Haji Khatibu Kai (CUF), kudai kuwa Wazanzibari wako tayari
kufa njaa kuliko kuendelea na Muungano aliodai hauna tija.
Mbunge huyo alitoa kauli hiyo jana bungeni wakati akichangia hotuba
ya bajeti ya Waziri Mkuu, alidai kuwa wananchi wa Zanzibar hawanufaiki
na Muungano wakati wanaonufaika ni watu wa upande wa Tanzania Bara.
Mbunge huyo alisema muungano huo umeiondoa Zanzibar katika ramani ya
dunia, hivyo ni bora ukavunjwa na kila upande ukaendelea kuwa nchi
inayojitegemea.
Hata hivyo, Mbunge wa Magomeni, Muhammad Amour Chomboh (CCM) alitoa
taarifa kwa Spika akidai kuwa kinachosemwa na mbunge huyo wa CUF ni
mawazo yake.
“Nataka kumpa taarifa mbunge mwenzangu kuwa Wazanzibari ambao ni
wazawa na wazalendo wa Zanzibar siyo kweli kuwa wanaukataa Muungano na
wala hawako tayari kufa kwa njaa kwa ajili ya kuukataa,” alisema
Chomboh.
Post a Comment