MRISHO NGASSA NJIANI KURUDI YANGA - TETESI HAI

MRISHO NGASSA NJIANI KURUDI YANGA - tetesi hai

Yanga wameendelea kuonyesha mabavu katika usajili baada ya kumsajili Kelvin Yondani, Nizar Khalfan, Barthez, Domayo na wengine wengi, leo taarifa za usajili kutoka klabu hiyo zinasema kwamba klabu hiyo ipo kwenye mazungumzo na klabu ya Azam ili kuweza kumsajili winga wa kimataifa wa Tanzania Mrisho Khalfan Ngassa.

Habari za ndani  zinadai kwamba Ngassa, Yanga na Azam wapo kwenye mazungumzo ya mwisho na huenda kesho kutakuwa na habari nzuri kwa wapenzi wa Yanga juu ya kurudi kwa kipenzi chao Ngassa mitaa ya Jangwani.
"Leo saa nne asubuhi Ngassa alifika pale makao makuu ya Yanga na akawa kwenye kikao kizito katibu wa Yanga na mmoja wa wadau wakubwa wa Yanga bwana Seif." - kilisema chanzo cha habari.

Katika usajili huo Yanga wapo tayari kulipa kiasi kikubwa cha fedha na kumtoa kiungo Nurdin Bakary ili kuweza kumtwaa winga huyo ambaye alishwahi kuichezea Yanga kwa mafanikio kalba ya kuhama kwa uhamisho uliovunja rekodi ya ndani ya usajili baada ya Azam kulipa milioni 60 kwa Yanga na kumtwaa Ngassa.
Chanzo:- Shaffihdauda blog

Post a Comment

Previous Post Next Post