NAIBU Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene asema: SIJAFUMANIWA!
NAIBU
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene, ameibuka na kukanusha
vikali uvumi ulioenea jana kuwa amefumaniwa na mke wa mtu mjini Singida
usiku wa kuamkia jana na kujeruhiwa mkono kwa kisu.
Akizungumza
na waandishi wa habari mjini Karatu jana jioni, Simbachawene ambaye pia
ni Mbunge Kibakwe (CCM) mkoani Dodoma, alisema habari hizo ni uongo na
kudai kuwa zimeenezwa na baadhi ya wabunge wa Chadema aliokutana nao
mjini Singida jana wakati akiwa njiani kwenda msibani Karatu.
Alisema
kuwa katika hoteli aliyofikia, kuna mtu alifumaniwa akiwa na mke wa
askari na kufafanua kuwa watu walizua jambo hilo kwa kuwa naye alilala
katika hoteli hiyo.
“Ni
uzushi tu walidhani kuwa mimi nimefumaniwa, ukweli ni kwamba jambo hilo
halijanitokea. Mimi nilifika hapa jana (juzi) nikitokea Dodoma kuelekea
Karatu kuhudhuria msiba wa shemeji yangu,” alisema Simbachawene.
Aliwataja
watu wanaodaiwa kueneza uvumi huo hizo kuwa ni wanachama wanane wa
Chadema akiwemo Mbunge wa Viti Maalumu kupitia chama hicho, Christina
Lissu.
“Baada
ya kufika Singida nilikwenda katika baa moja na kuwakuta wabunge wa
Chadema na baadhi ya wanachama, nilipata kinywaji na kurudi hotelini
kulala,” alisema Simbachawene.
Huku
akivua shati kuwaonesha waandishi wa habari kwamba hakukatwa mapanga
mikononi kama ilivyodaiwa, alisema kuwa alipoamka asubuhi ndipo alianza
kusikia habari kuwa amefumaniwa na mke wa mtu.
Awali
taarifa kutoka Singida zilizowekwa pia kwenye mitandao ya kijamii
zilidai kuwa Naibu Waziri huyo alikumbwa na mkasa huo jana alfajiri.
Tukio
hilo ambalo inaelezwa kuwa lilitoka majira ya saa kumi, baada ya
taarifa hizo kumfikia mwenye mke, ilimlazimu mmiliki wa hoteli hiyo
kutoa taarifa Polisi ili kuzuia maafa zaidi
Uvumi
huo ulidai kuwa baada ya taarifa hizo, iliwalazimu askari Polisi kwenda
katika hoteli hiyo ili kumuokoa Simbachawene, ambaye tayari alikuwa
amejeruhiwa mkono kwa sime na askari huyo mwenye mke.
Mara
baada ya purukushani hizo katika eneo hilo Naibu Waziri huyo alidaiwa
kwenda kutoa taarifa katika kituo cha Polisi mkoani Singida, ambapo
ilidaiwa kuwa katika maelezo yake aliandika jina la Josephat Joseph
badala ya kutumia jina lake halisi.
Hata hivyo, Mbunge Christina Lissu, alisema anashangazwa na taarifa za yeye kuhusishwa kueneza uvumi huo.
Alisema
walikutana na Naibu Waziri huyo, katika hoteli hiyo, wakiwa wanatoka
mkoani Tabora katika kesi na wabunge wa Chadema, Conchesta Rwamlaza,
Philipa Muturano na John Mrema ambaye ni Mkurugenze wa Bunge na
Halmashauri ya chama hicho.
“
Tulipofika Singida nilimwoa Simbachawene nimwita jina, alitufuata na
kutununulia vinywaji hapo hotelini,” alisema Lissu na kuongeza;
“Hata
tulipofika hoteli, baada ya muda tukasikia kutoka kwa mmiliki wa hoteli
akisema kuna watu wanataka kumharibia biashara. Tulipomuuliza kulikoni?
Akasema kwani hamna habari si mmewaona Polisi wakati mnaingia hapa,
huku akisema kuna kigogo wa Serikali amefumaniwa na mke wa askari.”
Kamanda
wa Polisi wa Mkoa wa Singida, Linus Sinzumwa alipoulizwa na Mwananchi
Jumapili alisema hakuna tukio kama hilo lililotokea mjini Singida wala
mahali popote katika mkoa huo.
“Huo
ni uzushi tu, hakuna tukio hilo mjini Singida na wala sijasikia taarifa
zozote za aina hiyo kutoka maeneo mengine mkoani hapa, alisema
Sinzumwa.
Chanzo; Mwananchi
Post a Comment