Tutashiriki mchakato wa katiba – Uamsho
Kutokana na sababu zilizotangulia kutajwa hapo juu na baada ya
mashauriano na viongozi tofauti katika jamii, Umoja wa Jumuiya na
Taasisi za Kiisilamu ndiyo imetoa uwamuzi wa kuwataka waumini na
wazanzibari wote kushiriki katika kutoa maoni lakini sambamba na uwamuzi
huo. Umoja wa Jumuiya na Taasisi za Kiisilamu, unapenda utoe tanbihi na
tahadhari ya hali ya juu kwa tume na kuitaka ifanye kazi yake kwa
uadilifu. Kwani uongozi pamoja na wazanzibari wengi kutokana na
udanganyifu wa tume zote zilizotangulia za uchaguzi, bado wasi wasi
mkubwa umetanda pamoja na imani ya kuwa haki haitotendeka. Vile vile
tunawasiwasi mkubwa wa mamlaka za nchi kupitia watu wachache wenye lengo
la kufanikisha maslahi yao binafsi, wataingilia utendaji wa tume na
shughuli zake kiutendaji kwa kuiburuza katika malengo binafsi na kwa
hilo hapa sisi viongozi wa umoja wa Jumuiya na Taasisi za Kiisilamu
tunatamka wazi kwamba hazitonyamaza kwa udanganyifu na dhulma yoyote
itakayofanyika na haitamstahamiliya wala kumuonea haya kiongozi yoyote
kwa dhulma hiyo.
JUMUIYA YA UAMSHO NA MIHADHARA YA KIISLAMU
(JUMIKI)
THE ASSOCIATION FOR ISLAMIC MOBILISATION AND PROPAGATION
P. O. BOX: 1266 -Tel: +255-777-419473 / 434145- FAX +255-024-2250022 E-Mail: jumiki@hotmail.com
MKUNAZINI-ZANZIBAR
24/06/2012
(JUMIKI)
THE ASSOCIATION FOR ISLAMIC MOBILISATION AND PROPAGATION
P. O. BOX: 1266 -Tel: +255-777-419473 / 434145- FAX +255-024-2250022 E-Mail: jumiki@hotmail.com
MKUNAZINI-ZANZIBAR
24/06/2012
Chanzo:-
Post a Comment