Kampuni ya Simu za Mkononi ya Vodacom Tanzania, imezindua huduma mpya ya
modem ya E173 kwa wateja wa malipo ya kabla ili kukidhi mahitaji ya
wateja wake.
Wateja wa Vodacom sasa watanunua modem aina ya E173 kwa Sh30,000 pungufu ya Sh5,000 ya bei ya zamani.
Wateja watapata kadi ya simu ya Vodacom na kufurahia MB 500 za mtandao wa 3.75 G bure kila mwezi ndani ya miezi mitatu
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Rene Meza, alisema huduma hiyo inalenga kuongeza wateja wanaopata huduma wake nchini, huku akisisitiza kuwa ni nafasi nzuri kwa vijana kutumia ofa hiyo kwa matumizi ya kila siku ya Internet.
“Tumeanzisha huduma hii nafuu ya internet kwa wateja wetu, huku bado Kampeni ya Wajanja Internet inaendelea, ambayo itawawezesha wateja kupata huduma ya Internet kwa Sh250 kwa siku,”. alisema Meza.
Ofa hiyo imekuja wakati Vodacom Tanzania ikiwa inatarajia kuwekeza zaidi ya Sh120 bilioni kuboresha mtandao, bidhaa na maendeleo ya teknolojia mpya za mawasiliano kwa mwaka huu.

Post a Comment