Mwigizaji Omotola Jalade wa pili kushoto akikabidhiwa zawadi na za
khanga, shanga na viatu Wema Sepetu wakati akiondoka kuelekea Nigeria
jana usiku. Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya One Touch
Solutions, Petter Mwendapole ambao waliratibu ziara ya msanii huyo.
Mwingine wa msanii Snura.
|
Omotola akijaribu bangili za kimasai alizopewa kama zawadi
Mwigizaji Wema Sepetu akimvalisha Khanga Omotola Jalade muda mfupi kabla ya hajandoka nchini kuelekea Nigeria.
|
MWIGIZAJI maarufu
kutoka Nigeria Omotola Jalade Ekeinde aliondoka nchini jana usiku na
kuahidi kusaidia soko la filamu nchini liweze kufikia ngazi za
kimataifa.
Akizungumza
na Mkurugenzi wa kampuni ya One Touch Solutions, Petter Mwendapole
iliyoratibu ziara yake pamoja na mwigizaji Wema Sepetu aliyekuwa
mwenyeji wake, Omotola alisema Tanzania ina kila sababu ya kuwika
kimataifa katika filamu.
“Kwa
Afrika Tanzania inaweza kuwa namba moja kama Nigeria, mna hali ya hewa
nzuri, vivutio vya utalii na pia mna waigizaji ambao wana vipaji, hii
inaweza kuwapeleka mbali yapo mambo madogo ya kurekebisha,” amesema.
Alisema
kwa kuanzia atafanya kazi kwa karibu na Wema Sepetu ambaye ndiye
alikuwa mwenyeji wake na kuhakikisha anafikia mafanikio ya juu katika
tasnia hiyo kwa kimataifa.
Omotola
mama wa watoto watatu, alisema kwa Nigeria yeye anafahamika kama Super
Star hiyo alipoambiwa anakuja kuzindua filamu ya jina hilo alijiona
kuwa ni muhisika wa moja kwa moja.
Tangu
kuwasili kwake nchini vyombo mbalimbali vya habari vya Nigeria
vimekuwa vikitangaza na kuzipa taarifa za uzinduzi wa filamu ya super
star nafasi kubwa.
Akiwa
nchini alitembelea kituo cha watoto yatima kinachohudumiwa na Tanzania
Mitindo House, kabla ya kula chakula cha mchana na watoto hao nyumbani
kwa Wema na jioni yake kuzindua filamu katika hoteli ya Giraffe. Pia
alitembelea jengo la Quality Plaza ambapo alikwenda kuangalia sinema.
Wakati akiondoka, Omotola alikabidhiwa Khanga, viatu vya kimasai na
shanga. Mbali na Wafanyakazi wa One Touch na Endless Fame na Image
Professional mwigizaji mwingine maarufu nchini na Mkurugenzi wa 5
Effect, Gabriel Mtitu alikuwepo uwanjani hapo kumsindikiza na
walizungumza mambo kadhaa
Post a Comment