YAW BERKO ASAINI MWAKA MMOJA YANGA

http://www.standardmedia.co.ke/images/friday/spocap080711_01.jpgKIPA namba moja wa Yanga aliyekuwa katika hatihati ya kuachwa, Yaw Berko, ameongeza mkataba wa mwaka mmoja.
Berko, raia wa Ghana, alikuwa katika orodha ya wachezaji wanaotaka kuachwa na Yanga iliyolenga kumnasa kipa Jean Ndoli, raia wa Rwanda.
Hata hivyo, kamati inayoshughulikia usajili, imefikia uamuzi wa kumuongezea Mghana huyo mkataba wa mwaka mmoja baada ya kufanya naye mazungumzo.
“Berko ana kiwango kizuri lakini amekuwa msumbufu, wanaoshughulikia usajili wamemuweka chini na kuzungumza naye,” kilieleza chanzo cha uhakika kutoka ndani ya Yanga.
“Ameonyesha ana nia ya kuendelea kuichezea Yanga, lakini ametakiwa kubadilika na kuachana na tabia ya kujiumiza makusudi au uzembe,” kiliongeza chanzo hicho.
Berko ni miongoni mwa makipa bora wa kiwango cha juu lakini wakati fulani aliwahi kulia anapigwa ‘misumari’ na kipa mmoja ambaye Yanga wameamua kumuacha.
Tayari Berko ameanza mazoezi na kikosi cha Yanga ambacho atakitumikia kwa msimu mmoja zaidi chini ya uangalizi.

Post a Comment

Previous Post Next Post