Zantel yanogesha Epiq Bongo Star Search Zanzibar
Huyu kijana alikuwa ni mmoja kati ya waliwakuna majaji
Mkuu wa Mawasiliano wa kampuni ya simu ya Zantel Awaichi Mawala
(kushoto) akiimba na wasanii waliokuwa wakisubiria kuitwa ndani kwenye
kuimba
Kundi kubwa la watu wakisubiria
Majaji wakifuatilia shindano hilo ambapo pia walitoa somo la muziki
Na Mwandishi Wetu
UWANJA
wa burudani uliopo katika eneo la Ngome Kongwe jana ulifurika maelfu ya
vijana waliojitokeza kushiriki katika kinyang’anyiro cha kuchaguliwa
kuingia katika fainali za shindano la Epiq Bongo Star Search 2012.
Huku
kukiwa na idadi kubwa ya washiriki wasichana pia kulikuwa na washiriki
ambao waliwasili wakiwa na vifaa mbalimbali vya kupigia muziki kama vile
gitaa,vinanda na vinginevyo ikiwa ni mikakati yao ya kujihakikishia
kuchaguliwa.
Akizungumzia
usaili wa Zanzibar Jaji Mkuu wa EBSS 2012 Ritha Paulsen alisema kuwa
ameguswa na mwamko wa washiriki kutoka Zanzibar.
‘Zanzibar ina vijana wengi wenye vipaji na ambao wanatakiwa kuendelezwa ili kufikia malengo yao katika muziki’ aliongeza Ritha.
Alisema
kuwa kupitia shindano la EBSS ambalo linadhaminiwa na kampuni ya simu
za mkononi Zantel anatarajia kupata vipaji vingi katika mikoa yote
ambayo usaili unaendelea.
Naye
Mkurugenzi wa Biashara wa Zantel kwa Zanzibar Mohamed Mussa mbali na
kufurahishwa na idadi kubwa ya washiriki waliojitokeza aliwataka vijana
wa kisiwani hapa kutambua kuwa muziki unaweza kuwapatia ajira kubwa.
‘Muziki
ni ajira, na ndio maana sisi Zantel tumeamua kuwekeza kwenye mashindano
haya ili kuwapa fursa vijana wengi zaidi’ alisisitiza bwana Mussa
Post a Comment