Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiwasili katika ukumbi wa MNelum Pokuna Mahinda Rajapaksa kuhudhuria ufunguzi rasmi wa Mkutano wa 58 wa chama cha Mabunge wanachama wa Jumuiya ya Madola (CPA) uliofunguliwa leo na Rais wa Sri Lanka Mhe. Mahinda Rajapaksa. Aliye pembeni yake ni Mjumbe wa CPA Tawi la Tanzania na Mbunge wa Kigoma Mhe. Zitto Kabwe.Rais wa Sri Lanka Mhe. Mahinda Rajapaksa akihutubia Maspika, Wabunge na maafisa zaidi ya 850 kutoka Mabunge ya nchi wanachama jumuiya ya madoloa wakati wa ufunguzi rasmi wa mkutano huo.
Spika
wa Bunge. Mhe. Anne Makinda akifuatilia kwa umakini ratiba ya ufunguzi
wa Mkutano wa 58 wa chama cha Mabunge wanachama wa Jumuiya ya Madola
(CPA) kabla ya ufunguzi rasmi leo Mjini Colombo Sri, Lanka, aliye
kushoto kwake ni Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Pande Ameir Kificho
na Mhe. Zitto Kabwe na aliye kulia ni Mhe. Mussa Azzan Zungu. Mkutano
huo umefunguliwa rasmi leo na Rais wa Nchi hiyo Mhe. Mahinda Rajapaksa.Spika
wa Bunge. Mhe. Anne Makinda akiteta jambo na Spika wa Baraza la
Wawakilishi Mhe. Pande Ameir Kificho pamoja na Mhe. Zitto Kabwe wakati
wa ufunguzi wa Mkutano wa 58 wa Chama cha Mabunge wanachama wa Jumuiya
ya Madola (CPA) leo Mjini Colombo, Sri Lanka. Mkutano huo umefunguliwa
rasmi na Rais wa Sri Lanka Mhe. Mahinda Rajapaksa. Wa Kwanza kulia ni
Afisa dawati wa CPA tawi la Tanzania Ndg. Said Yakubu.Mhe.
Zitto Kabwe akiteta jambo na Mbunge toka Uganda (hakufahamika jina mara
moja) pamoja na Spika wa Bunge la Malawi Mhe. Henry Chimundu Banda
(katikati) mara baada ya ufunguzi rasmi wa Mkutano wa 58 wa CPA
unaofanyika nchini Sri Lanka. Kulia ni Mhe. Hamad Rashid Mjumbe wa CPA
tawi la Tanzania.Spika
wa Bunge Mhe. Anne Makinda akishangaa jambo wakati wakiwa katika
mazungumzo na Spika wa Kenya Mhe. Kenneth Marende mara baada ya ufunguzi
rasmi wa Mkutano wa 58 wa CPA unaofanyika nchini Sri Lanka.Wajumbe wote wa Mkutano wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi rasmi leo.Picha na Owen Mwandumbya wa Bunge.
Post a Comment