Nyota Manchester City, Yaya Toure akiongozwa na ulinzi wa POlisi wa kutuliza ghasia uwanjani wakati wa vurugu hizo |
SENEGAL imeondolewa kwenye fainali
zijazo za Mataifa ya Afrika baada ya vurugu kubwa zilizofanywa na
mashabiki wake zilizosababisha kuvunjika kwa mechi dhidi yao na Ivory
Coast.
Mawe, chupa na silaha nyingine
zilirushwa na mashabiki uwanjani kabla ya Polisi kutumia mabomu ya
machozi kutuliza ghasia hizo mjini Dakar.
Shirikisho la Soka Afrika (CAF)
limetangaza kwamba Ivory Coast imepewa ushindi wa mabao 2-0 na itafuzu
kwa ushindi wa jumla wa 6-2.
vurugu |
Mechi hiyo ilivunjika dakika ya 78, huku
Ivory Coast ikiwa inaongoza mabao 2-0, shukrani kwa mshambuliaji wa
zamani wa Chelsea, Didier Drogba, aliyefunga mabao hayo yaliyosababisha
vurugu.
Kutolewa huko kwa Senegal, kunawakosesha
nyota wawili wa Newcastle, washambuliaji Demba Ba na Papiss Cisse fursa
ya kushiriki michuano hiyo itakayofanyika Afrika Kusini Januari
mwakani.
Lakini pia upande wa pili, kufuzu kwa
Ivory Coast, ni pigo kwa mabingwa wa Ligi Kuu, Man City ambayo itawakosa
Yaya na Kolo Toure, wakati Arsenal itamkosa Gervinho na Newcastle
Cheick Tiote.
Kolo Toure akiwa amezibwa na Polisi
SOURCE: http://www.dailymail.co.uk
Post a Comment