Madaam
Ritha akikata utepe wakati wa uzinduzi wa album ya Gospel ya Paschal
Cassian.Madaam Ritha alitoa kiasi cha shillingi Million 10 ili kufanikisha
malengo ya Cassian
|
“Nimekuwa
maskini baada ya Freemason kunifilisi na kuniletea mabalaa mengi katika familia
yangu.” Hivyo ndivyo anavyoanza kuzungumza Mshindi wa Bongo Star Search
(BSS)mwaka 2009 Paschal Cassian.Cassian ambaye ni muimbaji wa muziki wa injili,
anaeleza mkasa mzima kuwa baada ya kutoka BSS alipigiwa simu na watu waliomtaka
akutane nao ili wazungumze.Anasema alionana na watu hao na katika vikao vyao,
ndipo walipomueleza azma ya kumtaka kujiunga na Freemason.
Anasema,
alikaa vikao na hao na kufika eneo ambalo hukutana na ambapo alipokutana na
Watanzania wengi wakiwemo wacheza filamu, wachungaji na manabii.Anasema alipewa
mikataba mbalimbali na alitakiwa kutoa kafara wazazi wake ndipo alikataa.Kwa
mujibu wa Cassian, walimpatia nafasi ya kuchagua kitu anachotaka kutoka nacho
ambacho kitampa umaarufu, lakini sharti likiwa kuua wazazi wake ndipo
alipokataa.
Anasema
kama angekubali angeingizwa katika chumba maalum alichooneshwa ili kufanya kafara
hizo.Cassian anasema, anamjua Mungu na anamuamini na kama isingekuwa hivyo
asingeweza kutoa siri za Freemason kwani ukisema siri zao kwa ujasiri
hawakudhuru, lakini ukionesha hofu watafanya hivyo.
Anasema
baada ya kukataa kutoa kafara alivamiwa mara nne katika studio yake
aliyoifungua iliyokuwa ikiitwa Matunguri Fleva akiibiwa vitu vyenye thamani ya
sh milioni 12 na yeye kupigwa mara nyingi hata kufikia hatua ya kulazwa mara
kwa mara tena akiwa hoi.Anasema, kitu ambacho hatasahau ni matukio ya mara kwa
mara ikiwemo kukumbwa na mafuriko na kupoteza vitu vyote alivyonunua na vingine
maji yaliviondoa vitu vyote vya ndani na familia yake ilisaidiwa na watu
kuiokoa.
Matukio
anayoyapata anasema yanatokana na yeye kuachana na Freemason.“Wanakuja kiroho
na wakikushidwa wanakuja kimwili kwani wanakuwa na watu wengi, malengo yao ni
kukamata dunia nzima na wanawawezesha kifedha huku wachungaji wakiwawezesha
nguvu za kufanya miujiza kwa baadhi yao.
“Wapo
watu wengi, wachungaji, watu maarufu na marafiki zangu wapo na wengine
waliokuwa washiriki Bongo Star wana magari kwasasa yaani watu wanaibuka tu na
utajiri usiofahamika wala kueleweka.“Unapatiwa nguvu hata za miujiza kutoka
kwao kwani wao wanauwezo wa shetani kuwatambua kwa nembo zao,” anasema.Anasema
kuwa ujio wa filamu yake mpya itafunua mambo yote ya Freemason kwani yeye
alishajiunga na watu hao.
Cassian
anasema, filamu yake itakuwa tofauti kwani itahusiana na maisha ya watu wa
ndani na mambo aliyokutana nayo huko ikiwa ni pamoja na wachungaji walioko
Freemason na masupastaa.Cassian aliyezaliwa miaka 24 iliyopita mkoani
Mwanza,Wilaya ya Kwimba, anasema kabila lake ni mMsukuma na katika familia yao,
wapo watoto wengi sana zaidi ya 100 kwani baba yake ameoa wake wengi sana,
lakini kwa mama yake ni mtoto wa mwisho kati ya watoto nane.
Kuhusu
harakati za uimbaji, anasema alizianzia shuleni baada ya hapo anasema kuwa
alienda kusoma muziki Uganda kwa miaka miaka miwili na kurudi jijini Mwanza
kwaajili ya kufundisha kwaya mbalimbali za mjini humo.Kutokana na kutaka
kujulikana ulimwenguni, ndipo akajiunga katika mashindano ya kutafuta vipaji
yaitwayo bongo Star Search kwa mara ya kwanza na kuibuka mshindi.Anasema kuwa,
alikuwa muumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato kabla hajaokoka na awali
alikuwa muislam akiitwa Mohamed.
Akiwaelezea
waimbaji wa injili anasema: “Waimbaji wa injili wengi wananichukia kwa mtindo
wangu hasa waliotangulia waimbaji wengi hawana roho ya Mungu kwani kukupokea ni
ngumu na hata kukuelekeza pia ni ngumu,” anasema. Anaendelea kusema kuwa,
mwimbaji aliyeonesha ushirikiano wakati anatoka BSS ni Bony Mwaitege ambaye
aliwahi kumpa ushauri.
Pia
anadokeza kuwa amekuwa akisikia kwa watu kuwa Mwaitege analalamika kuiga mtindo
wake wa uimbaji, lakini haamini jambo hilo kwani Mwaitege ndiye amekuwa mshauri
wake katika uimbaji.
Akiizungumzia
albamu yake mpya anasema yenye nyimbo nane, ikiwemo ‘Wasamehe bure iliyobeba
albamu hiyo, lakini pia kuna nyimbo inayokamata mashabiki inayoitwa ‘Chuki ya
nini’? Anasema, ameimba huo kwa sababu haoni kwanini wanachukiana wakati wote
wanafanya huduma ya kumtumikia Mungu.
Albamu
hiyo anasema amerekodi katika studio ya Feature Sound japo alishatapeliwa na
baadhi ya mameneja hali iliyofanya aamue kusimama yeye kama yeye.Kuhusu ushauri
wake kwa waimbaji wenzake, ni kutiana moyo hasa waimbaji wakubwa kwani wao
wametangulia wasifanye muziki kama pesa, vipaji ni vingi ikiwemo kuacha
visingizio vya kutowapa tafu chipukizi.
Paschal Cassian enzi za Bongo star search 2009 |
Akiwaasa
wanamuziki wengine wanaoingia kwenye Gospel Music Cassian alisema“Watu wasije
kwenye nyimbo kwa ajili ya pesa kwani huu ni wito na kuna changamoto nyingi
sana, wasitarajie kupata pesa kwa haraka bali wajipange kimungu zaidi na wajitoe
katika roho.
Cassian
ameoa na ana watoto wawili Ritha na Anitha huku akitaja mafanikio aliyoyapata
ni kumjengea mama yake nyumba. Zaidi ya hilo amejenga nyumba yake kwa milioni
18, iliyopo jijini Mwanza pia akimiliki studio huku akifahamika ndani na nje ya
Tanzania.Anasema, amefahamiana na viongozi mbalimbali kiasi kwamba anaingia
sehemu yeyote na kusikilizwa shida yake akisema yote hayo ni baada ya kukutana
na Madam Ritha.
Na
Happiness
Mnale
Post a Comment