Ile beef kati ya Lunduno (Tamaduni Muzik) la Dar es salaam na Weusi
wa Arusha imerejea tena baada ya hivi karibuni Nikki Mbishi kuanza
kuwatupia madongo Weusi.
Jana kupitia ukurasa wake wa Facebook, Mbishi aliisambaza picha ya
Joh Makini iliyoleak mtandaoni ambapo rapper huyo anaonekana akiwa
kwenye usingizi mzito na msichana kwenye guest.
Katika picha hiyo kuna maneno yasemayo, “Joh Makini wa Mandugu Diggy
leta za moto…leta MANUVAAAAAA…mi ni shabiki mkubwa sana wa huyu
jamaa…big up kwake aendeleze HARAKATI mpaka madada zetu wakome.”
Haijulikani kama ni Nikki ndiye aliyeandika.
Kitendo hicho kimewakera wengi hasa kwakuwa kimefanywa na Nikki
Mbishi ambapo watu wanamlaumu kwa kutafuta beef ya lazima na Weusi ambao
mara nyingi wamekuwa kimya.
“I can see tamaduni muzik wanaluz direction,m ua fan bt that way is
not ryt kwanini ni nyie na weusi tu?acheni utoto let ua talents work
instid of beefs zisizo na kichwa wala miguu guys,” aliandika shabiki
mmoja.
Wakati huo huo jana kupitia Facebook, Nikki ameudiss wimbo mpya wa
Bonta wa kundi la Weusi uitwao ‘Tukutane Maktaba’ kwa kuandika, “Haya
sasa twende ki-CONSCIOUS mpaka “TUKUTANE MAKTABA”….#Hahahahaha another
WACK SHIT#”
Post a Comment