Marubani
wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) wakiwa wanafanya ukaguzi wa
mwisho kabla ya kuanza safari ya kutoka Kigoma kuenda Dar es Salaam leo
asubuhi. Hii ni baada ya wahandisi wa
shirika hilo kukamilisha kufunga kioo kipya ambacho kimenunuliwa kutoka
nchini Marekani. Ndege hii aina ya Dash-8 Q300 yenye namba za usajili
SH-MWF ambayo ilisitisha safari zake za Kigoma baada ya kioo cha mbele
katika chumba cha marubani kupata ufa (Wind shield crack) tarehe 11
Januari, 2013, muda mfupi baada ya ndege hiyo kuruka kutoka Kigoma
kurudi Dar Es Salaam katika safari zake za kawaida, imeanza tena safari
za Dar-Kigoma-Dar kulingana na ratiba .
Kapteni
Maqbool Sange akiwa ndani ya chumba cha marubani akifanya ukaguzi wa
mwisho wa ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) aina ya Dash-8
Q300 .Ndege hiyo leo imetua katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere ikitokea Kigoma ikiwa imebeba abiria 22. Uongozi wa Shirika imedhibitisha kuwa safari za Dar-Kigoma-Dar zitaendelea kama ratiba inavyosema.
Abiria
wakipanda ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) katika uwanja wa
ndege wa Kigoma, tayari kwa safari ya kuelekea Dar es Salaam.Picha Kwa Hisani ya Full Shangwe Blog
Post a Comment