Rais
Dkt. Jakaya Kikwete akiweka
shada la maua kwenye jeneza
Mzee
Amos Kaguta
na
kutoa heshima zake za mwisho.
|
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete jana(Feb 24,2013) aliungana na mamia ya wananchi wa Uganda katika
kushiriki Mazishi ya Mzee Amos Kaguta(97) Baba ya Rais Yoweri Museveni wa
Uganda,yaliyofanyika katika kijiji cha Rwakitura,magharibi ya Uganda.
Rais Kikwete aliwasili katika mazishi hayo
akitokea Addis Ababa mji Mkuu wa Ethiopia alipokuwa huko kuhudhuria Mkutano wa
viongozi wa cnhi za Maziwa Makuu uliokuwa na lengo la kutafuta amani ya kudumu
katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Akitoa
salamu zake za RambiRambi katika msiba huo Rais Kikwete alisema kuwa Watanzania
wapo pamoja na ndugu zao wa Uganda wakati huu wa majonzi na kusema kuwa yeye
binafsi anampa pole Rais Museveni na familia yake na kumtaka awe na moyo wa
subira katika kipindi hichi na kumuombea marehemu.
Rais
Museveni alimshukuru Rais Kikwete kwa kufika katika msiba huo ambapo alisema
kuwa Marehemu Mzee Amos atakumbukwa kwa kuthamini elimu ambapo aliwapeleka
watoto wake shule na kwa kufanya mabadiliko ambapo alikubali kufuata njia bora
za ufugaji wenye tija jambo ambalo ni gumu kwa wazee wengi wenye umri wake.
Rais
Museveni alitumia fursa hiyo kuwaasa vijana kuwatunza vyema wazazi wao ili
waishi muda mrefu na kulaani tabia ya baadhi ya vijana kuishi kwa kutegemea
mali za wazazi wao badala ya kuzalisha mali yao wenyewe akiongeza kuwa wazee
wana hazina kubwa ya maarifa kutokana na kukumbana na changamoto nyingi katika
maisha yao.
Marehemu Mzee Amos Kaguta alizaliwa mwaka 1916
katika kijiji cha Kabahambi,Kikoni Mtungamo nchini Uganda. Rais Kikwete na
ujumbe wake akiwemo Waziri wa Ulinzi Mh.Shamsi Vuai Nahodha waliondoka kurejea
jijini Dar es Salaam baada ya mazishi hayo
إرسال تعليق