Ndege zisokuwa na rubani zatumika Mali

Mapigano nchini Mali
Marekani inatumia ndege za ujasusi zisokuwa na rubani kuwasaidia wanajeshi wa Ufaransa na Umoja wa Afrika kupigana na wapiganaji wa Kiislamu wa Mali.
Afisa mmoja wa jeshi la Marekani alieleza kuwa ndege hizo, yaani drones, hazitakuwa na silaha na zitaongozwa na wanajeshi kama 100 wa Marekani kutoka nchi jirani, yaani Niger.
Hatua hiyo inafuatia juhudi za Marekani za kupambana na wapiganaji wenye uhusiano na Al Qaeda kaskazini na magharibi mwa Afrika.
Chad inasema kuwa wanajeshi wake wamekuwa wakipambana vikali na wapiganaji katika eneo la milima kaskazini mwa Mali.
Inaarifiwa kuwa wapiganaji kama 65 na wanajeshi 13 wa Chad wameuwawa.
- BBC

Post a Comment

Previous Post Next Post