BAYERN MUNICH VS BARCELONA: BARCA HAWAJAWAHI KUIFUNGA BAYERN JIJINI MUNICH - ILA HAWAJAFUNGWA UJERUMANI KWA MIAKA 11

Klabu za Ujerumani mara nyingi huwapa wakati mgumu wapinzani wao wakiwa kwenye ardhi yao, lakini Barca, ambao leo wanacheza na Bayern Munich wana rekodi nzuri katika ardhi ya Ujerumani. Hawajawahi kupoteza mechi katika kipindi cha miaka 10 iliyopita ndani ya Ujerumani - wakicheza mechi nane dhidi ya vilabu vya Bundesliga.

Hizi ndio mechi za Champions League walizocheza Barca dhidi ya vilabu vya Bundesliga.

2011/12: Bayer Leverkusen-FCB (1-3). Raundi ya kwanza ya hatua ya 16.

2009/10: Stuttgart-FCB (1-1). Raundi ya kwanza ya hatua ya 16.

2008/09: Bayern-FCB (1-1). Raundi ya pili ya robo fainali.

2007/08: Schalke-FCB (0-1): Raundi ya kwanza ya robo fainali.

2007/08: Stuttgart-FCB (0-2): Makundi

2006/07: Werder Bremen-FCB (1-1). Makundi.

2005/06: Werder Bremen-FCB (0-2). Makundi.

2002/03: Bayer Leverkusen-FCB (1-2). Makundi.

Miaka 11 baada ya kipigo

Inabidi urudi nyuma mpaka msimu wa 2001/02 kwa mara ya kwanza FC Barcelona walipoteza mchezo nchini Ujerumani, dhidi ya Bayer Leverkusen katika hatua ya makundi (2-1). Tangu wakati  Barcelona hawajafungwa na klabu ya Ujerumani, wakiwa na rekodi ya nzuri nyumbani na ugenini, wakishinda mechi 14 na suluhu 3.

Hawajashinda jijini Munich

Ukisoma hapo juu utaona hali nzuti tu kwa upande wa Barca, lakini rekodi ya Barca ndani mji wa Milan sio nzuri sana, vijana wa Tito Vilanova hawajawahi kushinda mechi yoyote rasmi dhidi ya Bayern ndani ya mji Munich. Walitoka sare kwenye nusu fainali ya UEFA Cup 95/96 na pia kwenye robo fainali ya Champions League  2008/09. Mara ya mwisho walifungwa na Bayern kwenye hatua ya makundi msimu wa  98/99.

Post a Comment

Previous Post Next Post