Kuvaa sidiria kunadhoofisha na kulegeza matiti

 Kwa mujibu wa utafiti uliofanyika nchini ufaransa, kuvaa sidiria kunadhoofisha “ligaments” au mishipa ya matiti na kusababisha matiti kulegea, au “sagging” CBS News imeripoti. Profesa Jean-Denis Rouillon wa Chuo Kikuu cha Hospitali ya Bensacon, amechapicha matokeo ya utafiti uliofanyika chuoni hapo, unaosema kuwa kuvaa sidiria kunaongeza matiti kulegea. “Matokeo ya utafiti yamethibitisha kwamba fikra kuwa sidiria ni mahitaji ni potofu” Profesa Rouillon amenukuliwa akisema. “Kiafya, kimaumbile na kifiziolojia, sidiria inadhoofisha matiti.” Sababu imeelezwa kuwa misuli ya mwili huwa inadhoofika na kuwa legelege kama isipotumika mara kwa mara. Ndio maana miguu, mikono, vifua n.k vya wanamichezo au watu wanaofanya mazoezi mara kwa mara huwa vimeimarika kuliko watu wenye mazoea ya kukaa chini kwa muda mrefu bila kuishughulisha misuli yao. Tatizo la kuvaa sidiria ni kwamba inayabeba au inayasapoti matiti na kuzuia mishipa ya matiti na misuli inayoyazunguka kushindana na mvuto wa dunia au “gravity,” hivyo kuinyima misuli na mishipa hiyo nafasi ya kufanya mazoezi. Matokeo ya misuli na mishipa hiyo ya matiti kukaa muda mrefu bila kufanya kazi, ni kulegea na kudhoofika zaidi. Mama mmoja anayeitwa Sharon amekubaliana na utafiti huo na kutoa maoni ya fuatayo: “I have a tremendous amount of experience on this subject. The last time I wore a bra was 1974. It has become obvious over the years that my breasts have not started to sag like other 57 year olds. Wearing a bra means that the breast muscles are not used. Therefore, sagging. When breasts are held up naturally by your muscles, the breasts sag less.” Kuna online kampeni inayoitwa “burnyour bra” au “choma moto sidiria yako.” Kampeni hiyo katika nchi za magharibi kama USA, Uingereza n.k. ni harakati za wasichana kutovaa sidiria na kutuma picha zao wakionyesha wamevaa blauzi bila sidiria. Pichani ni mmoja wa wasicha na hao aliyetuma picha yake.
 


Post a Comment

Previous Post Next Post