Ule
msemo wa ‘don’t judge the book by its cover’ unaoana sana na hiki
nachotaka kushare na wewe hapa. Hii ni gari yenye muonekano wa kawaida
sana kwa nje tofauti kabisa na muonekano wa ndani wenye hadhi ya vyumba
vya hoteli za nyota 5 ‘5 Star hotel suite’.
Kampuni ya kutengeneza magari ya kifahari Lexani Motorcars ya
California, Marekani imesema imetengeneza gari hiyo ‘Mercedes-Benz B6
Sprinter’ maalum kwaajili ya usalama wa mtu binafsi.
Gari hiyo yenye muonekano wa hadhi ya juu kwa ndani ina huduma zote
muhimu kikiwemo choo cha kisasa, sinki lililopambwa kwa dhahabu, jiko
dogo na viti vya leather. Gari hiyo pia ina kabati ndogo kwaajili ya
kuning’iniza makoti na kuifanya kuwa na muonekano wa ‘high-end yachts’
au ‘private jets’.
Gari hiyo pia ina TV ya Apple, Samsung LED TV, Bose surround sound
audio system na vingine. Inasemekana bei ya gari hiyo inaweza kufika
$450,000 ambayo ni zaidi ya Tsh Million 700.
Hivi ndivyo ilivyokuwa kabla haijatengenezwa kwa ndani
Post a Comment