Msanii
wa muziki na filamu Tanzania Hemed PHD ameamua kuachana na swala la
kuvaa hereni katika filamu zake baada ya wadau na mashabiki wake
kumwambia halina uhalisia.
Kutokana na kusikikia malalamiko mengi kutoka kwa mashabiki, Hemedy ameamua kuwa mpole na kufuata kile watakacho.
“Kumekuwa na fight kubwa sana kati ya mimi na director wangu pale
ninapokuwa na scene za ofisini nakuwa mbishi sana swala kuvaa hereni
sasa nimepata ushauri kutoka kwa mashabiki wangu nimeona nikamshauri
director wangu kuepuka kero ambazo hawazipendi mashabiki wangu. Nitakuwa
mjinga nisipo wasikiliza mashabiki wangu,” PHD aliiambia Enewz ya EATV
Post a Comment