Shirika la Umeme nchini (Tanesco), limesema idadi ya Watanzania walioomba kuunganishiwa umeme kwa kipindi cha miezi saba kuanzia Januari mwaka huu, imefikia 192,000 huku 80,000 wakiwa tayari wameunganishiwa.
Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Msemaji wa Tanesco, Badra Masoud, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu shughuli zinazofanywa na shirika hilo ikiwa ni pamoja na mikakati ya uboreshaji wa huduma.
Alisema tangu serikali itangaze kupunguzwa kwa gharama za kuunganishiwa umeme, mwitikio wa Watanzania ni mkubwa kiasi cha kuifanya Tanesco kupungukiwa na vifaa.
Alisema Tanesco ni kuwaunganishia umeme Watanzania 150,000 kwa mwaka, lakini tangu Januari idadi ya waliounganishiwa inafikia 80,000 huku 112,000 wakiwa wameshalipia na wanasubiri kuunganishiwa.
Serikali kupitia wizara ya Nishati na Madini, mwaka huu ilitangaza kupunguza gharama za kuunganishiwa umeme ili kuongeza idadi ya Watanzani wanaotumia nishati hiyo kufikia asilimia 30 ifikapo mwaka 2015.
Gharama za kuunganisha umeme vijijini katika umbali usiozidi mita 30 bila nguzo sasa ni Sh. 177,000 na kwa mijini niSh 320,000 badala ya Sh. 455,108 za zamani
Post a Comment