Mkulima wa Kenya, Mzee Isai akionesha rundo la mirungi lililokatwa kutoka mti wake wenye umri wa miaka 300 katika Jimbo la Meru. [Na Simon Maina/AFP] |
Na Julius Kithuure, Nairobi
Wanasiasa, wakulima na wasafirishaji wa Kenya wanatoa wito kwa serikali
kuanza mazungumzo ya haraka na Uingereza kuhusu marufuku inayokuja juu
ya mirungi, au miraa, mmea ambao unatoa athari za kuchangamsha
yanapotafunwa.
Marufuku ya Uingereza inaweza kusababisha kuporomoka kwa sekta ya kilimo cha mirungi cha mamilioni mengi, watetezi wasema.
Hapo tarehe 3 Julai, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uingereza Theresa May
alitangaza kwamba nchi yake inapanga kupiga marufuku mirungi, licha ya
maombi kutoka kwa Baraza la ushauri la Uingereza la matumizi Mabaya ya
Madawa kuwa mmea huo usipigwe marufuku, kwa kusema kuwa hauna uhusiano
na uhalifu mkubwa wa kupangwa.
Hata hivyo, May alisema kuwa sababu kuu za serikali yake kuamua kuupiga
marufuku zilikuwa za kisiasa, kama ilivyo nchi nyingi za Ulaya, pamoja
na Marekani na Canada ambazo zimeupiga marufuku mmea huo.
Mwanamume wa Kisomali akitafuna mirungi
huko Uithoorn, Uholanzi, tarehe 12 Januari, 2012. Serikali ya Uholanzi
hapo tarehe 10 Januari ilipiga marufuku majani hayo yanayochamsha,
yanayotumiwa zaidi na watu kutoka Somalia, Ethiopia, Kenya na Yemen. [Na
Koen Van Weel/ANP/AFP]
"Kukosa kuchukua hatua za maamuzi na kubadilisha msimamo wa kisheria wa
Uingereza kuhusu mirungi utaiweka Uingereza katika hali mbaya ya kuwa
nchi pekee, kitovu cha kanda cha kupatikana na biashara isiyo halali ya
mirungi," alisema katika taarifa bungeni.
"Kukamata mirungi inayopitia Uingereza ikiwa njiani kuelekea Uholanzi
tayari kumeongezeka kiwango na mara nyingi tangu pale Uholanzi
ulipoipiga marufuku mapema mwaka huu."
Licha ya ukosefu wa uwezo wa baraza la la ushauri kutoa ushahidi wa
mwisho wa athari zinazodaiwa za mirungi, May alisema kuwa ina madhara
kwa jamii.
"Mirungi inaendelea kuwa kipengele maarufu miongoni mwa madhara ya
kiafya na kijamii, kama vile kiwango cha chini na kuvunjika kwa familia,
kama ilivyotajwa na jamii zilizoathirika na polisi na viongozi wa
maeneo wanaofanyakazi pamoja nao," alisema, akiongeza kuwa kumilki
mirungi kunapaswa kuchukuliwa kwa namna ile ile kama kumiliki bangi, na
maonyo na faini kabla ya kukamatwa.
Mirungi na uchumi wa Kenya
Kupiga marufuku mirungi Uingereza kunaweza kuwa na athari hasi kwa
uchumi wa Kenya, wabunge wa Meru na na wafanyabiashara waonya.
Sekta ya kilimo cha mirungi inaajiri zaidi ya wakulima na
wafanyabiashara 500,000, kwa mujibu wa Utafiti wa Kiuchumi wa Kenya
uliotayarishwa mwaka 2012 na Ofisi ya Taifa ya Takwimu ya Kenya (KNBS).
Mirungi ni bidhaa ya nne ya Kenya ya usafirishaji katika vipengele vya
ujazo, kwa thamani ya karibu shilingi bilioni 16.5 (dola milioni 189),
kwa mujibu wa data za KNBS.
Wabunge na viongozi wa biashara ambao wanawakilisha mikoa ambako mirungi
inalimwa wamekosoa kile walichokisema kuwa ni kusita kwa serikali
kutetea kuifanya mirungi kua ni zao la fedha badala ya dawa.
"Kitu pekee tunachotaka ni kwa serikali yetu kuanzisha mazungumzo na
serikali ya Uingereza ili waweze kuzuia marufuku juu ya mirungi, ambayo
ni [chanzo] cha kujipatia riziki kwa watu wa Meru na Kenya kwa jumla,"
alisema Kimanthi Munjuri, mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa
Miraa wa Nyambene.
Kabla ya Uholanzi kupiga marufuku mirungi hapo mwezi Januari, Uingereza
ilikuwa soko la pili la miraa kimataifa kwa ukubwa, linaloagiza tani 20
hadi 25 kwa wiki za mirungi iliyolimwa Kenya. Sasa, Uingereza
inawakilisha muagizaji mkubwa zaidi, ikichukua tani 30 za mirungi kutoka
Kenya, Munjuri aliiambia Sabahi.
Nchini Uingereza, watumiaji wakubwa wa mirungi ni wahamiaji kutoka Somalia, Kenya, Ethiopia na Yemeni.
Kipkorir Menjo, mkurugenzi wa Jumuiya ya Wakulima wa Kenya, alisema kuwa
serikali za Uingereza na Kenya zinahitaji kufahamu athari za marufuku
ya mirungi.
"Maelfu ya wakulima, wafanyabiashara, wasambazaji na wasafirishaji
watabaki hawana kazi na hii sio habari njzuri wakati serikali ya Jubilee
inakabiliwa na ukosefu wa ajira," aliiambia Sabahi. "Sekta yote
inaelekea kuporomoka kwa sababu Uingereza ni soko kuu ambalo limekuwa
likiwaleta watu wetu mapato makubwa, na wakati huo huo kuipa nchi fedha
zakigeni zinazohitajika sana."
Wabunge wa Kenya wazishinikiza Uingereza, Kenya kupitia upya marufuku
Gavana wa Kaunti ya Meru, Peter Munya, na Seneta Kiraitu Murungi wameapa
kuwaongoza wanasiasa kupiga kampeni kwa serikali ya Uingereza kuipitia
upya marufuku hiyo.
"Mirungi inasaidia mamilioni ya maisha nchini Kenya," Murungi aliiambia
Sabahi. Alisema alikuwa anajitayarisha kuishawishi serikali ya Uingereza
kupambana na marufuku ya mirungi. "Pia ninapanga ujumbe wa kumuona Rais
[Uhuru][ Kenyatta juu ya suala hilo hilo hivi karibuni."
Tarehe 25 Julai, Munya na Murungi waliwasilisha ombi la malalamiko
kwenye Balozi wa Uingereza nchini Kenya, Christian Turner, wakiomba
kuondolewa kwa marufuku na kuanzishwa kwa majadiliano juu ya vipi
kuimarisha usalama katika matumizi ya mirungi.
Wanasiasa wa Kaunti ya Meru pia wanatishia kuhamasisha wakulima wa
mirungi na serikali kushinikiza kufungwa kwa vituo vya mafunzo ya
kijeshi vya Uingereza na mashamba yanayomilikiwa na Uingereza, pamoja na
kugomea bidhaa zinazoingizwa nchini kutoka Uingereza.
"Hata hivyo, nina matumaini kuwa haitafikia hatua hiyo," alisema
Florence Kajuju, mwakilishi wa wanawake kwa kaunti ya Meru katika Bunge
la Taifa. "Tuna imani kwamba bunge la Uingereza [halitashikilia marufuku
hiyo] wakati muda utakapowadia. Pia tuna matumaini kwamba rais wetu
ataingilia kati kwa kutuma ujumbe wa biashara kukutana [na] maofisa wa
serikali ya Uingereza."
Watunga sheria pia waliilalamikia serikali ya Kenya kubadilisha msimamo
wake kuhusu mirungi, kwani Mamalaka ya Taifa ya Kampeni Dhidi ya
Matumizi ya Dawa za Kulevya (NACADA) imeorodhesha mirungi kama dawa za
kulevya.
Tarehe 29 Julai, Mtandao wa Kidunia wa Wahusika wa Kiwanda cha Miraa na
wanasiasa wa eneo la Meru walifungua kesi katika mahakama kushtaki
NACADA. Mlalamikiwa anataka mirungi kuainishwa kama zao na kwa watunga
sheria kupitisha sheria inayotaka wizara ya kilimo kuitetea.
Jambo lililotia maudhi na serikali ya shirikisho walikataa kuingilia
kati, watunga sheria wameunda kamati ya wajumbe 29 kuchunguza athari za
kiafya za mirungi na matokeo yake kiuchumi katika Meru mahali ambapo
kiburudisho hicho kinalimwa.
"Tutachunguza masuala yote yanayohusiana na mirungi kwa kina," Kajuju
aliiambia Sabahi. "Hatutaacha kitu bila kushughulikiwa na ninaahidi
kwamba tutazingatia na kupitia tena matokeo ya tafiti zote na kutoa
mapendekezo bungeni ndani ya kipindi cha siku 90."
Biashara ya mirungi yaleta changamoto ya usalama
Wachambuzi wa masuala ya usalama na waangalizi wanasema jambo muhimu na
linaloleta hofu liko katika mjadala kuhusu mirungi -- biashara yake
inazalisha kiasi kikubwa cha fedha kisichohesabika.
Kiasi hicho hakipitii katika mfumo wowote halali wa kibenki na kutoa
mianya ya uwezekano wa kupatikana fedha za ugaidi na wenye siasa kali
katika Pembe ya Afrika, alisema Paul M. Taiti, mchambuzi mwandamizi
katika Kituo cha Taarifa za Usalama Nairobi.
Matumizi makubwa ya mirungi kwa wanamgambo kama al-Shabaab nchini
Somalia na al-Qaeda nchini Yemen yameleta kichochezi cha sifa mbaya
sana, aliiambia Sabahi.
"Wakati wote kuna shaka ambalo bado halijathibitishwa inayounganisha
mamilioni ya dola zinazoongezeka kutokana na biashara ya miraa
kugharimia mitandao ya ugaidi katika Pembe ya Afrika na
kaskazini-magharibi mwa Afrika," Taiti alisema. "Hii ndiyo maana Umoja
wa Ulaya na Uingereza wana wasiwasi na biashara nzima ya mirungi."
Chanzo - sabahionline.com
Post a Comment