Sasha akiwa na mtoto anayedai amezalishwa na Diamond |
Another
day, another scandal. Wiki hii Diamond Platnumz ameendelea kutawala
vichwa vya habari vya blogs na magazeti ya udaku na kugeuka version ya
Tanzania ya Justin Bieber.
Wakati ambapo prince huyo wa Bongo Flava hajazijibu tuhuma
zilizotolewa dhidi yake na Dayna pamoja na Baba Levo kuhusu wimbo wake
mpya, Number 1, lingine limeibuka tena. Kwa mujibu wa moja ya magazeti
ya udaku ya kampuni ya Global Publisher, ameibuka msichana aitwaye Sasha
Juma anayedai kuwa amezaa na Diamond.
Msichana huyo anadai alikutana na Diamond Mlimani City jijini Dar es
Salaam na akampenda kwakuwa anafanana na mpenzi wake wa zamani Wema
Sepetu. Linasema hawakuchukua muda na wakaanza uhusiano uliowafanya
wakutane kimwili na kupelekea msichana huyo kushika ujauzito.
Gazeti hilo linadai Sasha alimpa taarifa staa huyo ambaye alimuomba
asitoe mimba kwakuwa atamsomesha msichana huyo aliyefukuzwa shuleni na
pia kuahidi kumlea mtoto huyo.
“Ni kweli nimezaa na Diamond. Mtoto ana miezi mitatu sasa. Unajua
yeye ndiye alinikatisha masomo na kusema kuwa ataniendeleza na atamlea
mtoto hivyo alivyokaa kimya sikuona tena sababu ya kumfuatilia kwa vile
kwetu napata kila kitu,” gazeti hilo limemnukuu Sasha.
Limesema lilipomtafuta Diamond kwa simu ambaye kwa sasa yupo nchini
Kenya, alijibu: Hahahaaa…mbona hiyo ishu ni kubwa sana kwangu! Ukweli
huyo mwanamke simjui kabisa. Lete stori nyingine achana na hiyo.”
Bongo5 imezungumza na mchumba wake Diamond, Penny ambaye amekiri
kuisoma taarifa hiyo kwenye mtandao wa Global Publisher na kudai kuwa
haijamshtua kwa lolote kwakuwa scandal kama hizo hazimuumizi kichwa na
kwamba huja na kupotea
Post a Comment