Dk Massawe: TPSF iko sahihi kuhusu ugawaji mpya wa vitalu vya gesi, mafuta

 
PictureDk A. Massawe
Mwandishi: Dk A. Massawe – Mhandisi migodi ‘strategist in minerals and energy systems engineering’
Maoni yangu kuhusu mada ya, “Ubinafsi/Ufisadi wa Mengi na Chuki/Fitina kwenye Maendeleo” iliyotolewa na “CCM TANZANIA” ya Septemba 7, 2013 ni kama ifuatavyo:

Taasisi ya sekta binafsi (TPSF) iko sahihi kuhusu ugawaji mpya wa vitalu vya gesi na mafuta

Ukweli ni kwamba ni kuwa na hati miliki ya mtaji asilia ulioko kwenye raslimali za madini na sio kuwa na mtaji makaratasi kunakowezesha makampuni makubwa ya kimataifa kuendelea kujitajirisha kutokana na raslimali kubwa za madini zilizoko kwenye nchi zinazoendelea. Mtaji makaratasi unaohitajika kufanikisha ugunduzi na uvunaji wa raslimali za madini kama gesi asilia na mafuta ni kidogo sana ukilinganisha na mtaji asilia ulioko kwenye raslimali hizo za madini.

Hivyo, Serikali za nchi zinazoendelea zenye utajiri mkubwa wa madini zinapotoa hati miliki za raslimali zake za madini kwa makampuni ya kigeni zinawezesha makampuni hayo kujipatia mtaji mbegu makaratasi unaohitajika kwenye ugunduzi na uvunaji wa raslimali husika kwa njia ya kugawa sehemu kidogo tuu ya shea za hati miliki za raslimali madini husika kwenye masoko ya mtaji na hisa au kuziweka reheni ili kujipatia mikopo kwenye mabenki.

Serikali za nchi zinazoendelea zinapotoa hati miliki za raslimali zake za madini kwa makampuni ya kigeni zimewezesha makampuni hayo kutumia sehemu kidogo tuu ya mtaji asilia ulioko kwenye raslimali hizo za madini kama mtaji makaratasi unaohitajika kwenye ugunduzi na uvunaji wake kwa kushirikiana na


makampuni mengine ya kigeni, masoko ya mtaji na hisa na mabenki kunakochangia mapato kidogo sana ya kodi na misaada kwa hizo nchi zinazoendea ambazo huzidi kudidimia kwenye dimbwi la umaskini raslimali zake za madini zisizokuwa endelevu zinapozidi kupungua bila kuchangia vya kutosha  kwa ajili ya maendeleo yake. 

Ushauri uliotolewa na taasisi inayowakilisha sekta binafsi ya Tanzania kutaka ugawaji wa vitalu vipya vya utafutaji na uvunaji wa raslimali zetu za gesi asilia na mafuta usubiri huku utengenezaji wa sera na sheria mpya ya gesi asilia na mafuta inayowezesha wazawa kushiriki ili kufaidika zaidi ukiharakishwa ni mzuri tuu kwani kutumia sera iliyopitwa na wakati kwenye ugawaji uliopangwa kunamaanisha kwamba sera mpya inayoandaliwa haitarajiwi kuleta mabadiliko yoyote makubwa yenye manufaa ya watanzania. 

Mtaji asilia ulioko kwenye raslimali kubwa ya gesi asilia na mafutu tarajiwa iliyoko bado mikononi mwa watanzania inatosha sana kuwezesha watanzania kujipatia sehemu kubwa ya mtaji mbegu unaohitajika kwenye utafiti na uvunaji wake kwenye masoko ya mtaji na hisa na mabenki. Hii inawezekana iwapo serikali ya Tanzania itafanya uamuzi sahihi wa kutoa hati miliki za vitalu hivyo vya gesi asilia na mafuta kwa makampuni ya watanzania yanayohusisha sekta za umma na binafsi ili kuyawezesha kugawa au kuweka rehani sehemu kidogo tuu ya shea za hati miliki ili kujipatia mtaji mbegu makaratasi unaohitajika kwenye ugunduzi na uvunaji wa raslimali hizo  utakaowezesha Tanzania ifaidike zaidi na ugunduzi na uvunaji wa raslimali zake.

Shea nyingi zaidi za hati miliki ya raslimali kubwa za  madini kama gesi asilia, mafuta, urani na dhahabu zikiwa mikononi mwa watanzania zitawawezesha kuwa ndio watakaoamua ni lini na  vipi mtaji asilia ulioko kwenye raslimali zao za madini husika utavunywa ili kuleta manufaa makubwa zaidi kwao.

Kwa mfano Tanzania haipashwi kutoa vibali vya uvunaji au kutoa misamaha ya kodi ili kuharakisha uvunaji wa rasimali fulani za madini wakati kiwango cha mahitaji na dhamani yake kwenye masoko bado sio kizuri.

Badala yake, kama watanzania wangekuwa na shea nyingi zaidi za hati miliki, zingewawezesha kufanya uamuzi sahihi wa kuzibakiza ardhini raslimali za madini zilizogundulika hadi hapo dhamani yake kwenye masoko itakapokuwa kubwa vyakutosha kuewezesha uvunaji wake uwe na faida kubwa zaidi kwa Tanzania.

Wakati raslimali zilizogundulika zikiende kuhifadhiwa ardhini hadi wakati utakapokuwa mzuri kwa uvunaji wake, Tanzania inaweza kutumia  shea za mtaji asilia ulioko kwenye  raslimali hizo za madini yaliyohifadhiwa ardhini bado mikononi mwake kama rehani ya kujichukulia mikopo kwa ajili ya uwekezaji wa kujitafutia faida kwingineko.

Zoezi la kutumia raslimali iliyohifadhiwa ardhini kama reheni ya kuchukulia mikopo na kuirudisha mara kadhaa kwa faida huwezesha Tanzania ijipatie mtaji faida mkubwa zaidi kuliko hata mtaji asilia ulioko kwenye raslimali ya madini inayotumiwa kama reheni kuchukulia mikopo ambayo bado iko ardinni mikononi mwa Tanzania.

Shea nyingi za hati miliki za raslimali kubwa za urani zilizogundulika hapa nchini zingekuwa mikononi mwa watanzania zingekuwa zimewapa fursa nzuri zaidi ya kuamua kuzibakiza ardhini hadi hapo toknolojia ya uvunaji, uandaaji na utumiaji wake kwa ajili ya uzalishaji wa nishati itakapokuwa imeboreka na kuwa salama zaidi, Tanzania itakapokuwa tayari kuitumia kwa ajili ya uzalishaji wa umeme na soko lake duniani litakapokuwa limeimarika zaidi.

Hoja ya kwamba Mzee Mengi kahodhi hati miliki za vitalu vingi vya ardhi kwa ajili ya utafutaji wa madini bila kuvifanyia kazi kunakosesha mapato kwa serikali na ajira kwa watanzania sio sahihi kwani huenda hata raslimali ya madini yanayotafutwa haipo kwenye vitalu alivyomiliki na ukweli ni kwamba utafutaji wa madini ni sawa na mchezo wa bahati nasibu unaotoa wezekano kidogo sana kwa mchezaji kugundua raslimali inayovunika ya madini yanayotafutwa na hivyo mchezaji kutakiwa kumiliki viwanja vingi zaidi ili kuongeza kiwango cha uwezekano wa kupata  madini yanayotafutwa kama kivutio kwenye harakati za kutafuta mtaji makaratasi unaohitajika kuviendeleza kwenye masoko ya mtaji na hisa na mabenki.

Viwanja vya utafiti wa madini alivyomilikishwa mtanzania au mtafiti mwingine yeyote kufanyiwa au kutokufanyiwa kazi kunatokana na ubora wa viwanja husika na mahitaji na bei ya madini yanayotafutwa kwenye masoko, yaani kiwango cha uvutio wa viwanja husika kwa masoko ya mtaji na hisa na mabenki kuwekezeaa mtaji makaratasi unaohitajika kuviendeleza.

Iwapo hali bado sio nzuri, utafiti kwenye viwanja alivyomilikishwa mtafiti itabidi usubiri hadi hapo vitakapokuwa kivutio kwa wawekezaji mtaji makaratasi unaohitajika kuwekezea.

Itakuwa ni makosa makubwa sana kuwahimiza watafutaji wa kitanzania kutumia mtaji wao wenyewe kwenye utafutaji mkubbwa wa madini hapa nchini kwani kutokana biashara ya utafutaji wa madini kuwa sawasawa na mchezo wa bahati na sibu unaotoa uwezekano kidogo sana kwa mchezaji kufanikiwa kupata bila ya kuhusisha viwanja vingi vya utafiti na mtaji mkubwa sana ambao mtu mmoja mmoja hataweza kuwa nao. Badala yake, serikali makini hutarajiwa iwe  ikiwahimiza na kawawezesha watafutaji wa madini wa kizalendo wawe wakijitafutia sehemu kubwa zaidi ya mtaji unaohitajika kwenye masoko ya mtaji na hisa na mabenki kwa kugawa kwa wengine au kuweka reheni sehemu kidogo tu ya shea za hati miliki za utafutaji madini  walizopewa na serikali.

Tatizo hapa ni wengi huko serikalini na mitaani kutokuelewa vizuri biashara ya madini inavyofanya kazi na kuwa na imani potofu kuwa ni makampuni makubwa ya kigeni pekee yenye mitaji mikubwa ya makaratasi yanayostahili kumillikishwa vitalu vya ugunduzi na uchimbaji wa raslimali za gesi asilia na mafuta hapa nchini na sio watanzania wenye mtaji wote wa asilia kwenye raslimali hizo za madini ambao hawana mtaji makaratasi wa kutosha kwa ajili ya kuzviendeleza ambao ni  sehemu kidogo sana ya mtaji asilia walio nao kwenye raslimali zao za gesi asilia na mafuta.

Kabla ya kulielewa jambo kwa kina, sio vyema kupuuza na kubeza shauri zitolewazo na watanzania kama mtu mmoja mmoja au taasisisi zao kwa serikali yao kwa nia njema ya kuisihi ifikirie upya maamuzi yake kwa lengo la kuyaboresha kwa manufaa yetu sote.

Post a Comment

Previous Post Next Post