Mshindi wa ulimbwende wa Marekani 2014 aandamwa na wabaguzi

Picture
2014 Miss America
Picture
2007 Miss Tanzania
Nilipoisoma habari hii kwenye NPR, imenikumbusha kwetu Tanzania ambako tuliwahi kumpata Miss Tanzania mwenye asili ya India na katika hali isiyoshangaza sana, akaandamwa na wabaguzi wa rangi kuwa si Mtanzania halisi hata ikiwa amezaliwa na kukulia Tanzania.
The 2014 Miss America, Nina Davuluri, the 24-year-old Miss New York is the first contestant of Indian heritage to become Miss America; her talent routine was a Bollywood fusion dance.

Her pageant platform was "celebrating diversity through cultural competency."

The native of Syracuse, N.Y. wants to be a doctor, and is applying to medical
school, with the help of a $50,000 scholarship she won as part of the pageant title. Davuluri's victory led to some negative comments on Twitter from users upset that someone of Indian heritage had won the pageant. She brushed those aside.

"I have to rise above that," she said. "I always viewed myself as first and foremost American."
Nadhani wengi wetu tuna chembechembe za kibaguzi kwa kiwango fulani kulingana na historia, malezi na mahusiano yetu na watu. Wapo wanaowabagua wenzao kutokana na rangi ya ngozi zao, kiwango au aina ya elimu, tamaduni, imani na dini zao, makabila, vyeo, jinsi na jinsia, uwezo wa kiuchumi n.k.

Kwa mtizamo wangu, nadhani ubaguzi huchangiwa sana na ujinga (ignorance) kuhusu kile anachokibagua, na kama ilivyo ada ya kuondoa ujinga, ni lazima mtu akubali na awe na nia ya kujifunza zaidi kuhusu kile asichokifahamu. Kwa kiasi fulani, watu walioweza kubadilika kutoka kuwa wabaguzi wakubwa na kuwa wenye upendo, husimulia kuwa walifanikiwa baada ya kujifunza mengi kuhusu wale waliowabagua na hata ikiwa hawakukubaliana na yote waliyojifunza, walijenga tabia ya uvumilivu (tolerance) na kuishi ule usemi wa ‘mfanyie mwingine vile ambavyo ungependa ufanyiwe wewe, na usimfanyie yale ambayo pia usingependa ufanyiwe’, zaidi sana, ‘live and let live’.

Habari kamili ya Miss America 2014 inapatikana NPR.org

Post a Comment

أحدث أقدم