Obama atafuta uungaji mkono kushambulia Syria

Waandamanaji wakipinga hatua ya kijeshi dhidi ya Syria mjini New York
Waandamanaji wakipinga hatua ya kijeshi dhidi ya Syria mjini New York
Utawala wa  rais Obama unafanya msukumo mkali wa saa 48 ili kushawishi bunge na wananchi  wa Marekani kuunga mkono hatua ya kijeshi dhidi ya Syria.

Washauri wa ngazi ya juu wa kijeshi watafanya mikutano ya faragha  na ya wazi na wabunge wiki hii. Rais atafanya mahojiano na mitandao mikubwa 6 ya televisheni  leo Jumatatu  kabla ya kutoa hotuba ya White House kwa taifa Jumanne usiku.


Utawala  wa Obama pia unasambaza  kanda za  video kwa washirika wake, wabunge wa Marekani na mashirika ya utangazaji  zikionyesha raia wa Syria ambao ni waathiriwa wa mashambulizi ya silaha za  kemikali.


Maafisa wa Marekani wanasema wana ushahidi ambao unathibitisha  pasipo shaka kwamba jeshi la Bashar Al Assad lilishambulia wapinzani wa serikali kwa gesi ya sumu  katika maeneo ya Damascus mwezi uliopita na kuuwa zaidi ya watu 1,400.

Post a Comment

Previous Post Next Post