LEO JUMAPILI SEPTEMBA 08, 2013 KATIKA KIPINDI CHA INJILI SWAHILI RADIO
Muasisi
na aliyekuwa Askofu Mkuu wa Kanisa la EAGT Marehemu Dkt. Moses Kulola
enzi wa Uhai wake. Mtangazi wako Mary Mgawe anazungumzia wasifu na
mazishi ya aliyekuwa Askofu Mkuu wa kanisa la EAGT (EVANGELISTIC
ASSEMBLIES OF GOD TANZANIA) Dkt. Moses Kulola nchini Tanzania mwishoni
mwa mwezi uliopita Tanzania ilikumbwa na msiba wa kitaifa baada ya
kumpoteza Askofu Dkt. Moses Kulola, aliyetambulika na wengi kama
Baba,Babu, na hata mlezi wa mafunzo ya kiroho katika maisha ya watu
wengi.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakitoa heshima
za mwisho na kuweka udongo katika kaburi la aliyekuwa Muasisi na askofu
Mkuu wa Kanisa la EAGT Marehemu Dkt. Moses Kulola wakati wa ibada ya
mazishi yake yaliyofanyika katika viwanja vya kanisa huko Bugando Mwanza
Septemba 4,2013.
Sikiliza
Swahili Radio Online Kipidi cha Injili na Mary Mgawe sasa hivi Baada
ya hapo miziki mchanganyiko ya Injili na kipindi kinarudiwa tena.
LINK
Tuko hewani masaa 24 tukiwatangazia kutokea Jijini Washington D.C. Marekani.
Post a Comment